Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya mabadiliko ya kurusha
matangazo yake ambayo yanaviwezesha vyombo vya habari (redio na tv)
kupata matangazo hayo moja kwa moja bila kufunga mitambo yao katika eneo
la bunge.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
cha bungeni imeeleza kuwa mfumo huo utakuwa ukirusha mtangazo kupitia
satellite ambapo vituo vya redio na runinga vitakuwa vikitumia satellite
kupokea matangazo hayo na kuyarusha katika vituo vyao.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa redio na vituo vya runinga vitakuwa vikiyapata
matangazo kupitia satellite Intelsat 17, nyuzi 66 upande wa Mashariki.
SATELLITE: Intelsat 17 @ 66 East
FREQUENCY: 11024.2500MHZ
SYMBOLRATE: 3071.8 Mbps
POLARIZATION: Horizontal
FEC: 1/2
MODULATION: 4PHASE-QPSK
AUDIO: CH. 1…noneI, CH.2…none, CH.3…TV Audio na CH. 4…Radio
Aidha
taarifa hiyo imeeleza kuwa mfumo huo ndiyo unaotumika na mabunge mengi
duniani na kutumika kwa mfumo huo hakuwazuii waandishi wa habari kwenda
bungeni kuchukua habari.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )