Muandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Dokta
Williama aliendelea kuwasikiliza wakuu hawa wa polisi ambao vyeo vyao
vinawatambulisha kama ma RPC kwenye mikoa yao.Lifti ikafunguka na wote
wakatoka ndani ya lifti.Askari hao wakaendelea kwa mwendo wa kasi na
kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.Dokta William akajiweka sawa nguo zake
na kuingia ndani ya ukumbi huu.Gafla macho yake yakatazamana na midomo
ya bastola alizo elekezewa na wakuu wa polisi waliokaa kwenye viti vyao
huku wakioneka kukasirishwa sana na uwepo wake
ENDELEA....
IGP bwana Gudluck Nyangoi akwaamuru wezake kuziweka silaha zao chini na wakati
“Karibu dokra Willian”
Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akitabasamu na kumfanya dokta William kushusha pumzi nyingi,kidogo wasiwasi ukaanza kumpungua.
“Jamani
huyu ni miongoni mwa wanajeshi wa umoja wa matiafa,yupo hapa nchini kwa
ajili ya mafunzo wa madaktari wa jeshi letu juu ya jinsi gani wanaweza
kumtengeneza sura bandia”
“Dokta,kwanza samahani kwa kukuvunjia ratiba zako kwa maana haikuwa katika ratiba zako leo kama nitakuitaji hapa”
“Bila samahani mkuu”
“Karibu ukae”
Dokta
William akaka kwenye kiti alicho onyeshwa na bwana Nyangoi,akawaytizama
makamanda wote waliopo ndani ya ofisi na hapakuwa na hata mmoja anaye
mfahamu zaidi ya IGP Gudluck Nyangoi.
“Jamani
kama munavyo jua,sisi kama jeshi la polisi tumekubwa na msiba mkubwa
sana wakupoteza vijana wetu katika tukio la jana usiku,Pia ni aibu kubwa
kwetu sisi kama jeshi la polisi kwa kushindwa kupambana na majambazi
ambao,sijajua ni vipi tulishindwa kuwazuia na kusababisha maafa makubwa
kama haya”
Ukimya
ukatawala,huku akili ya Dokta William ikiwa inajaribu kupanga kitu cha
kuzungumza kabla hajaulizwa kwani ametambua umuhimu wake wa yeye kuwa
hapa ni kuwashauri viongozi waliopo humu ndani
“Jamani
ninawasililiza,nasubiri maoni yenu.Nini tufanye ili kuwakamata hawa
watu na ninavyo sikia wao ni wasichana sasa sijajua inakuwaje wasichana
kama hawa wanatushinda kirahisi rahisi?”
“Mkuu
mimi ninaona,kwanza tudhibiti mipaka yote ya nchi jirani kwa maana
kumbukeni kulikuwa na tishio la kundi la Al-Shabab kuivamia mlimani
city.Sasa isije ikwa ndio hao wameanza kutekeleza mipango yao”
“Asante bwana Shaban Mbago,mwengine?”
“Mkuu
mimi kuna swala ambalo bado silipatii picha,haiwezekani mpango ule wa
kumsafirisha yele binti katika njia ya ardhini ulibumburuka.Swali ni
je,ni nani aliye toa siri ile?”
Mapigo
ya moyo ya dokta William yakaanza kwenda kasi,ila hakutaka kuiruhusu
hali hii kuendelea kuundama moyo wake,akawatazama wakuu wa polisi
waliopo eneo hili na kuwaona wengi wapo kimya kila mmoja akikosa cha
kuzungumza.Dokta William akanyoosha kidole na bwana G.Nyangoi akampa
ruhusa ya kuzungumza
“Wakuu wangu mimi ninajambo moja ninaomba nizungumze”
“Zungumza tuu,kwani ushauri wako ni mkubwa sana”
“Kuna
hali ambayo inaendelea ndani ya jeshi lenu,kwa kipindi kifupi nilicho
kaa katika nchi hii na kushirikiana na jeshi lenu nikagundua kuna hali
amayo sio nzuri na endapo mukiacha ikikua na kukomaa,Siku hadi siku
jeshi lenu litazidi kuzalilisha na kuteketea mwisho wa siku ile imani ya
kusema kuwa Tanzania ni nchi ya amani itafutika katika vichwa vya watu
wengi”
“Viongozi
kwa viongozi hamuaminiani,hilo ni la kwanza.Pili viongozi mumekuwa ni
watu wakuunda vikundi vikundi vya watu ambao munawatumia kwa maslai yenu
binafsi na si ya taifa.Kwa mfano kuna magaidi ambao jeshi la polisi
mulikuwa munawatafuta kwa kipindi kirefu sana.
Kutokana
na uaminifu finyu wa baadhi ya viongozi magaidi wale wakaendelea kudumu
na kuishi kwa kipindi kirefu pasipo serikali kuzungumza kitu cha aina
yoyote.Kila mulipo kuwa munajaribu kwenda kuwakama walikuwa wanawakwepa
na kubaki mukijiuliza mutafanya nini?”
“Kabla
ya hichi kikao kuendelea,jiulizeni je hakuna wasaliti watako vujisha
siri juu ya watu muna watafuta? Na kama wapo je kuna haja gani ya hichi
kikao kuendelea kuwepo hapa?”
Ukumbi
mzima ukakaa kimya,sura za makamanda wote wapolisi zikawa zikimtazama
Dokta William ambaye amezungumza maneno ambayo wengi wao hawakuwa
wanayafikiria kuyazungumza
“Musikalie
kuunda tume kuchunguza vitu ambavyo munajua majibu yake kabla ya
kuzungumza.Nyinyi ni jeshi,munatakiwa kuwa kitu kimoja na si kuwa katika
mgawanyiko ambao utawakost garama ambazo si za msingi.Jaribuni kuiga
baadhi ya mbinu za kijeshi katika mataifa makubwa yaliyo endelea,mfano
Marekani na kadhalika.Nitatolea mfano mdogo tuu wa wa wale wanejeshi
walio tumwa kwenda kumuua Osama Bin Laden,Gaidi ambaye sisi kama Israel
alituumiza pia vichwa jinsi ya kumpata”
“Ila
kikosi cha wanajeshi wachache walio tumwa kuumuua Osama,kilikuwa ni cha
siri kubwa hata makamu wa raisi wa Marekani hakuwa analifahamu
hilo,zidi ya raisi Obama na wasadizi wake,Na tukio zima lilipokuwa
linaendelea walikaa kwenye chumba maalumu pasipo na mtu yoyote kuwa na
mawasiliano ya simu ya mkononi,hata raisi mwenyewe alizuiwa kuwa na
simu.
Huo
ni mfano mdogo ila hapa hapa ninashanga muheshimiwa unaendeleza kikao
ila kuna huyo bwana hapo anachati na simu chini ya meza,Je kuna umuhimu
gani wa hichi kikao?”
Bwana Noel Muro akastuka na kuuingiza simu yake mfukoni baada ya kunyooshewa kidole na Dokta William.
“Muro ninaomba uzime simu yako”
Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akimtazama bwana Muro
“Mkuu cha mwisho kukizungumza ninawaomba,muunde kikosi maaalumu cha siri kitakacho wa pambana na hili swala.Asanteni”
Dokta William akakaa kwenye kiti na viongozi wote wakampigia makofi wakimpongeza kwa ushauri wake alio utoa.
“Dokta
Willim asante sana kwa ushauri wako mzuri sana.Mimi ningekuomba
usaidiane na mimi kuunda kikosi kitakacho weza kuwasaka hawa
majambazi.Nipo radhi kuwaishawishi serikali kuongezea mshahara”
Laiti
IGP bwana G.Nyangoi angegundua mtu anaye muomba juu ya huo mpango ndio
muhusika nambari moja wala asinge zungumza hayo maneno
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )