Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Evarist
Ndikilo atoe wiki mbili kwa wakuu wa taasisi za umma na za binafsi
wajieleze ni lini wataendeleza viwanja vya ofisi walivyopewa mjini
Kibaha.
Ametoa
agizo hilo jana Septemba 21, 2016 wakati akizindua Mpango Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania (2015 – 2020) na Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya
Tanzania, Kibaha, mkoani Pwani.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa huo kwamba kuna taasisi za umma na za binafsi ambazo zimepewa
viwanja vya kujenga Ofisi kwa zaidi ya miaka mitatu lakini zimeshindwa
kuviendeleza hadi sasa wakati kuna watu bado wana shida ya kupatiwa
viwanja.
“Kibaha
ni kimbilio la mkoa wa Dar es Salaam, kule kumejaa na hapa kuna nafasi
kwa hiyo hawa ambao hawajaendeleza waandikie barua leo hii hii na uwape
wiki mbili waeleze ni lini watakuwa tayari kuanza kazi hiyo.” – Majaliwa
Taasisi
hizo zilizotanjwa na Waziri Mkuu ni Hazina ndogo yenye viwanja viwili
ambapo kiwanja kimoja chenye namba 232 kimeendelezwa lakini kiwanja
kingine chenye namba 221 bado hakijaendelezwa.
Taasisi
nyingine na viwanja vyao kwenye mabano ni Chuo Kikuu Huria (kitalu na.
228), Njuweni Institute (kitalu na. 229), TANESCO (kitalu na. 218), TRA
(kitalu na. 233) na SF Group (kitalu na. 225). Vingine ni vya Benki ya
CRDB na TAKUKURU ambavyo hakutaja namba za vitalu vyake.
Majaliwa
alisema kuwa anajua kuna watu wa Serikali watasema hawana bajeti,
lakini Bunge la bajeti linaanza Aprili mwakani. Kwa hiyo, wajipange
kwenye bajeti ijayo, ili ifikapo Julai mosi, 2018 hawajafanya kitu,
wachukuliwe hatua.
“Tuchukue
viwanja vyetu tuwape wengine, na hawa wanaosuasua, tuwaache ili
watakapokuwa tayari waombe upya na tutawapa wakati mwingine,” Majaliwa.
Waziri Mkuu pia alimtaka Ndikilo awawekee deadline ya kujieleza katika barua hizo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )