Jeshi
la Zimbabwe limeonya kuingilia kati mgogoro unaoendelea kati ya
viongozi wa chama tawala cha ZANU-PF, baada ya Rais Robert Mugabe
kumfukuza kazi aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa.
Kamanda
wa Jeshi la Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga amefanya mkutano na
vyombo vya habari akiwa na viongozi wengine waandamizi 90 wa jeshi hilo
na kutoa onyo hilo.
Amesema endapo wapigania uhuru wataendelea kugombana kuhusu madaraka, jeshi hilo halitasita kuchukua hatua.
“Kung’olewa
madarakani kunakoendelea sasa, ambako kwa uwazi kunalenga wajumbe wa
chama ambao walipigania uhuru, lazima kusitishwe,” alisema Jenerali
Chiwenga.
“Tunawakumbusha wanaofanya hivi kuwa katika masuala ya kulinda mapinduzi yetu, jeshi halitasita kuingilia kati,” aliongeza.
Rais
Mugabe alimfukuza kazi Makamu wake wa Rais akieleza kuwa amekuwa
akiendesha kampeni ya chinichini ya kutaka kumrithi bila kufuata
utaratibu wa chama.
Pia, alidai kuwa Mnangagwa alienda kwa watabiri na waganga akitaka kujua ni lini Mugabe atafariki dunia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )