Rais
John Magufuli amewataka wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye na Hussein
Bashe, ambao michango yao bungeni imekosoa uendeshaji uchumi, wampelekee
majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi.
Wabunge hao wa Mtama na Nzega Mjini waliikosoa Serikali wakati wa kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye alishutumiwa na wabunge
hao kumpotosha Rais, alisema wakati akihitimisha mjadala huo kuwa
alipigiwa simu na mkuu wa nchi na kuelezwa hayo.
“Naomba
ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia
huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi,” alisema Waziri Mpango.
“Waziri,
mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka
sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway.
“Wawalete
hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au
Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge.
“Hayo
ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika will raise
up to this challenge from his excellence the president (wataifanyia kazi
changamoto ya mheshimiwa Rais.”
Akijibu
hoja za wabunge hao na wengine, Dk Mpango alisema si kwamba Serikali
imeiweka pembeni sekta binafsi bali bado haijakaa vizuri na wakati
mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )