Pamoja na kwamba spika Anne Makinda ametoa kauli kwamba, Zitto ambaye alikuwa mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini atapewa stahiki zake zote kama mbunge ambaye amelitumikia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa miaka 5, lakini Zitto ameliandikia bunge kupitia ofisi ya spika na kumtaka Spika kusitisha malipo hayo ambayo yamepangwa kufanywa kwake!
Maamuzi hayo ya mzalendo Zitto kukataa kuwa sehemu ya wabunge watakaolipwa pesa za kiinua mgongo hayakuonekana kuwashtua sana maofisa wa bunge kwani wengi wamemzoea Zitto kwa kupinga posho za vikao zinazotolewa kwa wabunge.
Itakumbukwa pamoja na CHADEMA kueleza katika sera zao kuwa posho za vikao bungeni ni haramu, na wanasisitiza kuwa kitendo cha kuipokea ni kuwasaliti Watanzania wa hali ya chini, lakini ukweli ni kwamba HAKUNA mbunge aliyetokana na CHADEMA hata mmoja ambae amewahi kukataa kupokea posho hizo za vikao zaidi ya Zitto kipindi akiwa CHADEMA!
Ni Zitto pekee ndiye hakuwahi kupokea hata shilingi ya bunge iliyotolewa kwa njia ya posho ya vikao. Hii ni kutokana na uoga wake wa kuwasaliti watu wa hali ya chini ambao ndio wanaumia inapotokea pesa nyingi ya walipa kodi kufujwa bungeni kwa njia za ugawaji wa posho za vikao na kiinua mgongo kwa wabunge.
Aidha, nitaambatanisha picha inayoonyesha barua hiyo kutoka kwa Zitto kwenda kwenye ofisi ya spika kwa lengo la kusitisha malipo ya kiinua mgongo yaliyopangwa kufanywa kwake june mwaka huu.
Ifahamike: Pesa ya kiinua mgongo utolewa kwa wabunge kutoka kwenye mfuko wa bunge na haina mahusiano na pensheni ya mbunge
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )