Featured
Loading...

Ajira Mpya Serikalini( TAMISEMI)......Wanahitajika watu 233

 


 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anakaribisha maombi ya kazi  kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mia mbili thelathini na  tatu (233) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili;
 

1.MHANDISI II UJENZI (HIGHWAY) – NAFASI 07 .

 SIFA ZA MWOMBAJI  
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/Sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi walioojiimarisha katika Ujenzi wa  Barabara (Bachelor of Science in Civil Engeneering – Highway) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.MHANDISI II UJENZI (STRUCTURAL) - NAFASI 134 .

 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi waliojiimarisha katika Miundombinu na Uimara wa Majengo (Bachelor of Science in Civil Engeneering - Structural) kutoka  
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

3.MHANDISI II (UMEME) - NAFASI 09 .

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Umeme (Bachelor of Science in Electrical  Engeneering) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

4. MHANDISI II UJENZI (BUILDING) - NAFASI 83

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/   Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi waliojiimarisha katika ujenzi wa  Majengo (Bachelor of Science in Civil Engeneering - Building) kutoka katika vyuo   vinavyotambuliwa na Serikali.

 ðŸ‘‰Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

TAKUKURU Wametangaza Nafasi 350 za Kazi....Bofya Hapa Kutuma Maombi

 


Mkurugenzi  Mkuu  wa  Taasisi  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  Rushwa  (TAKUKURU) anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kuajiriwa katika nafasi za kazi zifuatazo:

1.1    AFISA UCHUNGUZI (NAFASI 200)
1.2   Sifa za Kitaaluma:
Muombaji awe angalau na elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotam­bulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika fani zozote kati ya hizi: Mambo ya  Kale na Utalii, Sheria, Uhasibu,Teknolojia ya  Habari, Elekitroniki, Misi­tu, Kilimo, Ununuzi, Uchumi na Mipango, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Takwimu, Utawala wa Umma/Serikali, Utunzaji wa Kumbukumbu, Usimamizi na Uthamini wa Ardhi, Mafuta  na Gesi,Ukadiriaji wa  Majenzi, Uhandisi wa  Umeme, Uhandisi kati­ka Kemia, Mifugo, Usanifu wa Majengo, Mambo ya anga, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Ujenzi na Uhandisi wa Maji;

2.1    MCHUNGUZI MSAIDIZI (NAFASI 150)
2.2    Sifa za Kitaaluma:
Muombaji awe na cheti cha elimu ya kidato cha nne (CSE) au kidato cha sita (ACSE). astashahada au stashahada ya fani yoyote inayotolewa na Taasisi au chuo kinachotam­bulika na Serikali ya Tanzania, pamoja na fani kama vile ujenzi, ulinzi, udereva, upa­kaji rangi, ufundi magari, vifaa vya muziki, utunzaji wa kumbukumbu , TEHAMA, maendeleo ya jamii, uhazili, menejimenti ya hotel , n .k.

 Mwisho wa kutuma maombi ni - 8th November, 2021 

 ðŸ‘‰Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

Majina Ya Wanafunzi waliopata mkopo Awamu ya pili ( Wanafunzi 7,364 ) .... Bofya Hapa Kutazama

 



Na Mwandishi Wetu,HESLB
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya pili yenye wanafunzi 7,364 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 19.4 bilioni kwa mwaka wa masomo 2021/2022 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Oktoba (22, 2021) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ilisema orodha hiyo iliyotolewa leo inafanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 45,095 yenye kiasi cha TZS 119.3 Bilioni.



Badru ameongeza kuwa HESLB imeanza kupeleka fedha za wanafunzi waliopangiwa mikopo katika vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account) na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili.

“Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni … lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wanaopangiwa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea ili watimize ndoto zao,”
 amesema Badru.

 Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu, Badru amesema imepangwa kutolewa Jumatatu, Oktoba 25, 2021 baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi unaoendelea na kuwataka waombaji mikopo kutembelea akaunti zao ya SIPA kupata taarifa kuhusu maombi yao.

“Orodha hii ya pili inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja … tunakamilisha uchambuzi wa maombi mengine na tutaoa orodha ya tatu katika siku tatu zijazo, yaani Jumatatu Oktoba 25, 2021,” amesema Badru.

Wakati huohuo, Badru amesema HESLB imeshapokea fedha kwa ajili ya malipo kwa wanafunzi waliopangiwa mikopo awamu ya pili  taratibu za malipo  zimekamilika na fedha za wanafunzi zinatarajia kufika vyuoni kuanzia leo Ijumaa, Oktoba 22, 2021.


 Kwa mujibu wa Badru, Serikali imetenga TZS 570 bilioni kwa ajili ya mikopo ya jumla ya wanafunzi 160,000. Kati yao, wanafunzi 70,000 watakuwa ni wanufaika wapya na wanafunzi zaidi ya 90,000 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka.

Aidha, Badru alisema HESLB inawasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea.

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 1097 (Mamlaka ya Mapato-TRA)....Bofya Hapa Kutuma Maombi




 VACANCY ANNOUNCEMENT

 On behalf of Tanzania Revenue Authority (TRA), Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) invites dynamic and suitable qualified Tanzanians to fill 1097 vacant posts mentioned below.

_________________


1. TAX MANAGEMENT OFFICER II -   NAFASI  294

2. TAX MANAGEMENT ASSISTANT II -NAFASI  326
 
3.CUSTOMS OFFICER II -  NAFASI 167

4.CUSTOMS ASSISTANT II NAFASI 114

5.PUBLIC RELATION OFFICER II – NAFASI  3

6. ICT TECHNICIAN II – NAFASI 30


7. ICT OFFICER II (COMPUTER SYSTEMS ANALYSIS AND DEVELOPMENT) - NAFASI 31.

8. ICT OFFICER II (NETWORK ADMINISTRATOR) –NAFASI  2 

________
 
 ðŸ‘‰Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

9. ICT OFFICER II (DATABASE ADMINISTRATION) - NAFAS 6 .

10. ICT OFFICER II (ICT SYSTEMS RISKS AND SECURITY) – NAFASI 6.

11. ICT OFFICER II (COMPUTER/BUSINESS APPLICATION SUPPORT) –NAFASI 6.

12. ICT OFFICER II (COMPUTER SYSTEM ADMINISTRATION) NAFASI 19.

13. ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) COMPUTER SYSTEMS ANALYSIS AND DEVELOPMENT– 1 POST

14. ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) DATABASE ADMINISTRATION – NAFASI 1.

15.  ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) SYSTEMS RISKS AND SECURITY-  NAFASI 1 .

16. RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II - NAFASI 18.

17. DRIVER II  NAFASI 59 .

18.  LEGAL COUNSEL - NAFASI 3

19 RATING IINAFASI 1 .

20.ACCOUNTS ASSISTANT II-  NAFASI 4 .

21. PERSONAL SECRETARY IINAFASI 5.

___________________

 Mwisho wa kutuma maombi ni - 4th November, 2021

Mbunge wa CUF Ataka Mwenge usikimbizwe Kwa Madai Kwamba Umepoteza Mvuto

Leo Jumanne Novemba 6, 2018, mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameuliza kama Serikali haioni kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa sasa hakuna umuhimu tena kwani umekuwa ukisababisha mambo mengi ikiwemo magonjwa ya zinaa ikiwamo HIV.

Akiuliza swali katika kikao cha kwanza, mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma, Mtolea alielekeza swali hilo kwa Waziri Mkuu kuwa kama Mwalimu Nyerere alisema anawasha mwenge ili uwekwe juu ya mlima Kilimanjaro kwanini serikali inaendelea kuutembeza.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde amesema "kuwa lengo la mwenge ni kujenga misingi ya binadamu na utu wa mtanzania, pia umelenga kuhamasisha ukombozi wa bara la Afrika, kupitia utaratibu huu, mwenge ni chombo muhimu kwa kuimarisha nchi yetu.”

Mara baada ya majibu hayo Mbunge huyo wa jimbo la Temeke alidai mwenge huo kwa sasa unapokelewa na baadhi ya watumishi wa serikali, wakiwemo madiwani pamoja wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari pekee akidai kuwa wananchi wamechoshwa kuuona kila mwaka.

Kufuatia swali hilo la Nyongeza Spika Ndugai aliamua kumkatisha mbunge huyo wa Temeke kwa kile alichokisema kuwa swali lake halikuwa la msingi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya November 7


Sakata la Mo Dewji Kutekwa laibuka bungeni

 
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ameibua suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji kiaina.

Akichangia mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2019/20 bungeni leo Jumanne Novemba 6, 2018 , Mchungaji Msigwa alisema wafanyabiashara hawako huru kufanya biashara nchini.
“Wawekezaji wanajionaje kuwepo katika nchi hii, wapo salama? Takwimu zinaonyesha wawekezaji wa nje wanafunga virago.

“Je wawekezaji wa ndani wakoje? Wana raha? Kama bilionea mkubwa nchi hii anaweza akashikwa, akafichwa, akaachiwa halafu hadi leo hajaruhusiwa kusema alikuwa wapi unadhani nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? Haya mambo hatuwezi kufumbia macho, lazima tuyajadili.”

Alisema hadi leo hakuna taarifa ni nani aliyemteka na pia alikuwa wapi na kuhoji  kwa sasa diplomasia ya nchi ikoje.

“Wakati wa Benjamin Mkapa (Rais wa Awamu ya Tatu) aliwahi kusema Tanzania inahitaji ulimwengu kuliko ulimwengu unavyotuhitaji sisi.”

“Kama leo Balozi wa Ulaya anaitwa nchini kwake kujadili mahusiano  kama taifa linahitaji kujiuliza wageni wanaionaje Tanzania. Wafanyabiashara wanafunga virago wanaondoka kwa sababu wanaona hawako sawa. Mheshimiwa Mpango, (Waziri wa Fedha na Mpango Dk Philip Mpango)  Serikali yako haieleweki inaendeshaje uchumi wa namna gani?” alihoji.

Aidha, alisema taifa linahitaji Katiba ambayo itawaunganisha Watanzania wote. Mwalimu Nyerere walipigana vita ya Uganda na wakashinda kwa sababu walikuwa wamoja,” alisema.

Alisema kinachowaunganisha Watanzania wote ni Katiba ili kuweza kupigana na kushinda vita ya uchumi.

Alisema wateule wa Rais wanamtii yeye tu na kwamba kila mtu ni kambale (samaki) na kwamba wakuu wa mikoa na wilaya hawawatii mawaziri.

“Mtu anatumia Instrument (vifaa) vya Serikali amekaa katika ofisi yenye bendera, polisi wanamlinda halafu mnasema hayo ni ya  kwake mwenyewe. Kama ni ya kwake mwenyewe kwa nini hamchukulii hatua?” alihoji.

Wakati akiendelea kuchangia, aliibuka Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel na kutaka kufahamu Chadema ilizungumza nini katika kikao walichokifanya kati yao na mashoga 40.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge,  Mussa Zungu alimpotezea Dk Mollel na kumtaka Mchungaji Msigwa aendelee kuchangia mpango huo.

Jeshi la Polisi: Tunaendelea Kumsaka Mpenzi wa Wema Sepetu



Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Liberatus Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.

“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.

Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.

Watanzania Kufaidi Matunda Ya Reli Ya Kisasa Mwakani.....Waziri Mkuu alidhishwa na kasi ya ujenzi, Asilimia 96 ya walioajiriwa ni Watanzania


MIUNDOMBINU ni muhimu katika maendeleo ya Taifa lolote ambalo linalohitaji kusonga mbele kiuchumi, kijamii kwa sababu husaidia Serikali katika kufanikisha malengo iliyojiwekea.

Miundombinu hiyo ambayo inalenga kuboresha na kuimarisha uchumi inajumuisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya uchukuzi na usafirishaji kama reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, ununuzi wa ndege na meli.

Kukosekana kwa miundombinu ya uhakika kunachangia kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kuongezeka gharama za uchukuzi.

Katika kutambua umuhimu wa miundombinu kwenye kukuza uchumi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujikita katika kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ili kuhakikisha Taifa linasonga mbele kiuchumi.

Mradi huo wa ujenzi wa mfumo wa reli mpya ya kisasa (SGR) unaojengwa na Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), unatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Mwanza ina urefu wa km. 1,219.

Jumamosi, Novemba 3 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa reli hiyo kuanzia eneo la Shaurimoyo (Dar es Salaam) hadi Soga (Pwani) ambapo alisema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi huo.

Alisema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 kinatarajiwa kukamilika Novemba 2019 na kipande wa cha kutoka Shaurimoyo hadi  eneo la Pugu chenye urefu wa km. 20 ambacho kilipangwa kukamilika Julai 2019, lakini kwa kasi ya mkandarasi kitakamilika Machi 2019.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii na kiwango hikihiki. Kazi mnayoifanya inavutia,” alieleza.

Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. Magufuli ya kutaka kuona SGR  inakamilika kwa wakati na kuanza kutumika nchini yanatimia kwani wananchi nao watakuwa wamerahisishiwa usafiri.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo kutaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani hususani ambazo hazijapakana bahari pamoja na kupunguza muda wa safari katika maeneo ambayo mradi huo unapita.

Pia  itasaidia katika kutunza barabara na kupunguza gharama za ukarabati wa mara kwa mara kwa sababu mizigo mingi itakuwa inasafirishwa kwa njia ya reli na maroli yatapungua barabarani, hivyo kuzifanya ziwe imara na kudumu.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa SGR inakwenda kukuza sekta zingine za kiuchumi nchini kwa sababu nazo zinategemea uimara wa miundombinu ya usafiri wa uhakika.

Katika  sekta ya viwanda reli hiyo itasaidia kusafirisha bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda mbalimbali na kuwafikia watumia kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Akizungumzia kuhusu suala la ajira katika ujenzi wa mradi wa SGR, Waziri Mkuu alisema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.

“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu, hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uadilifu na muwe mabalozi wazuri ili wananchi wengine waweze kupata ajira kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa nchini ikiwemo ya ujenzi.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli  kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.

Alisema awamu hiyo ya mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na njia kuu 205 ambazo km 95 zitakuwa zinapisha kitagharimu sh. trilioni 2.7.

“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422  na njia kuu 336 ambazo km 86 zitakuwa zinapishana kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5 chenye njia kuu 294 na km 73.5 zitakuwa zinapishana.

Kipande kingine ni cha kutoka Tabora hadi Isaka km 162.5 chenye njia kuu 130 na km 32.5 zitakuwa za kupishana na Isaka hadi Mwanza km. 311.25 njia kuu 249 huku km 62.5 zitakuwa za kupishana.”

Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa itachochea mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Mkurugenzi huyo alisema reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na uhakika.

“Kuchangia katika pato la Taifa na sera ya viwanda kwani mradi huo umeongeza mahitaji ya saruji, kokoto, nondo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi, hivyo kuvifanya viwanda vyetu vya ndani kupata soko la bidhaa zake.”

Akizungumzia mradi huo kwa ujumla, Mkurugenzi huyo alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha Morogoro-Makutupora.

Alisema jumla ya km. 722 za ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa kwa sasa zinatekelezwa katika vipande viwili, kipande cha Dar Es Salaam-Morogoro km. 300 kinajengwa kwa ubia wa kampuni ya YAPI MERKEZI ya Uturuki na MOTA-ENGIL ya Ureno na kipande wa Morogoro-Makutupora km. 422 kinajengwa na kampuni ya YAPI MERKEZI.

Kadogosa alisema katika mradi huo wa reli za kisasa mfumo wa uendeshaji wa treni utatumia nishati ya umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na tayari taratibu za kumpata mkandarasi za kujenga njia za umeme upo katika hatia za mwisho.

Kuhusu ujenzi wa madaraja Kadogosa alisema kazi ya ujenzi wa madaraja na makaravati unaendelea ambapo daraja refu katikati ya jiji la Dar es Salaam ina jumla ya urefu wa km. 2.56 na ujenzi wake umefikia asilimia 46.

 “Kuna madaraja ya kati 26 na makaravati 243, madaraja ya treni kupita juu yapo 17, madaraja ya treni kupita chini yapo 15 na madaraja reli juu ya reli yapo matano, pia jumla ya stesheni sita zitajengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, kati ya hizo kubwa zitakuwa mbili na nne zitakuwa ndogo.”

Alisema usanifu wa stesheni hizo umezingatia mazingira na asili ya Tanzania ambapo stesheni ya Dar es Salaam ina sura ya madini adimu ya Tanzanite wakati stesheni za kati usanifu wake umezingatia utamaduni na nyumba za asili na stesheni ya Morogoro itaonesha uhalisia wa milima ya Uruguru.

Kadhalika, Mkurugenzi huyo alizungumzia kuhusu ajira katika mradi huo ambapo alisema una jumla ya wafanyakazi 5,440, vibarua 4,743 ambapo jumla ya asilimia 96 ni Watanzania na asilimia nne ni wageni, wataalamu 189 wa Kitanzania na 258 wa kigeni kwa uwiano wa asilimia 42 Watanzania na wageni asilimia 58.

Pia jumla ya ajira 626 za Watanzania wasio na utaalamu na 19 za wenye utaalamu zimepatikana kupitia kampuni za wazawa (sub-contractors) wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huo.

Akizungumzia kuhusu ardhi na mali nyingine, Kadogosa alisema mali za wananchi wapatao 6,514 zenye thamani ya kiasi cha sh. bilioni 83.099 zitakiwa kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa reli kwa kipande wa Dar es Salaam-Morogoro.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 6, 2018.

DC Muro Awatia Mbaroni Watuhumiwa Watatu Walioshiriki Kumtoa Mimba Mwanafunzi


Na Imma Msumba Arumeru,
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Wilaya ya Arumeru limewakamata watuhumiwa wa Tatu ambao wameshiriki kumtoa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.

Dc Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego na kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na mtia mimba ambao wamefikishwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani

Akielezea jinsi alivyopewa ujauzito na kisha ujauzito kutolewa aikaeli Pallangyo amesema ni kweli alipata ujauzito Kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi nae Jirani nyumbani ambae alikuwa akimrubuni Kwa kumpatia fedha

Kwa upande wao watuhumiwa wa sakata hilo kijana aliempa mimba Binti,pamoja na mama Mzazi wa Aikaeli na mwanamke ambae ni ndugu wa Kijana aliempa mimba ambae anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito Binti wametoa sababu mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe Kwa zenyewe Kutokana na mama wa Binti kukiri Kuwafahamu watuhumiwa wenzake na kuelezea tukio la Mchezo mzima ulivyokuwa

Akidhibitisha taarifa Za Binti huyo kuwa mjamzito na kutoa ujauzito, Mganga mkuu wa halmashauri ya Meru Daktari Cosmas kilasara amesema vipimo vya awali vilionyesha Binti kuwa mjamzito na vipimo walivyofanya tena vimeonyesha Binti sio mjamzito tena ambapo amesema hata hivyo Binti huyo ameendelea kupata dalili zote Za kuwa na ujauzito ikiwemo ya maziwa kutoka.

Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya Usalama kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio hilo , ambapo pia amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi 57 Kwa kipindi Cha miaka miwili iliyopita.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru

Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali Imefanya Mambo Makubwa Sana Ndani ya Miaka Hii Mitatu


 
Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, imefanya jitihada kadhaa ikiwa ni sambamba na kutekeleza  sera mbalimbali ambazo zimeiwezesha nchi ya Tanzania kupata mafaniko makubwa ndani na nje ya nchi katika kipindi  cha miaka mitatu

Akizungumza  jana jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, ametaja mambo 10 muhimu  yaliyofanywa na  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu na ambayo yameitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.

Dkt. Abbasi alitaja mambo hayo kuwa ni uchumi unaoendelea kukua kwa kasi nzuri, ambapo  katika mwaka 2017/18 uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 7.1 na kuongoza katika nchi zote za Afrika Mashariki, huku  ukiingia katika rekodi ya kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi duniani kama ambavyo  ripoti mbalimbali za kimataifa zimeeleza.

“Uchumi wetu ni wa tisa kwa ukuaji wa kasi duniani na katika Afrika, Kusini mwa Sahara ni wanne, hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum ya mwezi  Machi, 2018 na kwa nchi za Afrika Mashariki  uchumi wa Tanzania unaongoza kwa ukuaji” alisema Dkt. Abbasi

Kuongezeka kwa mapato ya Serikali katika kipindi cha miaka mitatu, Rais Magufuli amethubutu kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza kasi ya kukusanya kodi na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya Serikali kutoka wastani wa shilingi  bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia wastani wa  shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.

Kufufuliwa kwa mashirika ya umma, Dkt. Abbasi alisema kuwa kutokana na ufuatiliaji, ubunifu, uwekezaji wa Serikali ya Rais Magufuli, mashirika mengi  mfano  Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL), Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamkala ya Maji Safi (DAWASA) na Bandari  sasa yameanza kuamka kuwa na ufanisi, kuongeza mapato na mengine kutengeneza faida.

“Baadaa ya Serikali kuchagiza mageuzi ya kiutendaji sasa  kwa mwaka TTCL  inakusanya shilingi bilioni 212 kutoka shilingi bilioni 102, Bandari imekusanya kutoka shilingi bilioni 703 hadi kufikia shilingi bilioni 838 kwa mwaka, TRC kutoka shilingi bilioni 23 hadi 36 kwa mwaka  na DAWASA shilingi bilioni 32.4 hadi shilingi bilioni 122.4 kwa mwaka “ alisema Dkt. Abbasi

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya  viwanda ambapo jumla ya  viwanda 3,306 viliandikishwa, na vingine vinaendelea kujengwa na baadhi vimekamilika. Halikadhalika viwanda hivyo vimeanza kutengeneza  bidhaa mbalimbali ambapo kati ya hivyo viwanda 251 ni vikubwa na vya kati ni 173.

Ambapo mchango wa ekta ya viwanda katika pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 5.2 mwaka 2015 hadi 5.5 mwaka 2017. Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikua kutoka asilimia 6.5 mwaka 2015 hadi asilimia 7.1 mwaka 2017/18.

Akiendelea kufafanua mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano Dkt. Abbasi alisema kuwa Rais Magufuli amepambana na rushwa na ufisadi kwa pamoja na mambo mengine, sambamba na  kutimiza ahadi yake ya kuunda Makosa ya Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi

“Mpaka sasa kesi mpya 41 zimefunguliwa, na  kuna maombi ya dhamana 346 yamewasilishwa katika Mahakama hii kati ya mwaka  2017 na 2018” alisema Msemaji huyo wa Serikali.

Katika sekta ya usafirishaji nako, Serikali ya Rais Magufuli imefanya mageuzi kadhaa, yaliyopelekea sekta hiyo kupata mafaniko  ya kuwa  na  ndege nne mpya zinazoendelea kuleta mageuzi katika usafiri wa anga nchini, abiria wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka kutoka takribani abiria 4,000 kwa mwezi hadi abiria 30,000 kwa mwezi.

Aliongeza kuwa  ndege mbili   aina ya Air Bus zenye uwezo wa kubeba abiria watu 132 zitawasili nchini Disemba mwaka huu, na ndege aina ya  Boeing dreamliner ya pili inatarajiwa kuwasili nchini Oktoba mwaka mwakani.

Aidha, mradi wa umeme wa Stigler’s gorge utakapokamiika unatarajiwa kuzalisha  megawati 2,100, sambamba na mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha standarg gauge kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na baade Dodoma, ambapo umefikia 33% ya ujenzi.

Mafaniko mengine ya Serikali hii yanaonekana katika katika sekta ya afya,  ikiwemo kujenga vituo vya Afya vya Kata 210 na kukarabati vingine vingi kufikisha idadi ya vituo vinavyotoa huduma hadi mwaka huu kuwa 7,746 kutoka vituo 7,014 mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 10.4.

 Dkt. Abbasi  alifafanua kuwa vituo hivi pia vina wodi za kina mama na vifaa vya kisasa. Aidha, ajira zaidi ya 6,000 za kada ya afya zimetolewa. Katika miaka mitatu Zahanati zimeongezeka kutoka 6,143 mwaka 2015 hadi 6,646 mwaka huu ikiwa ni sawa na  ongezeko la zahanati 503  ambapo baadhi zilijengwa na zingine kukarabatiwa sawa na ongezeko la asilimia 8.1.

Vilevile, Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi ya kiutendaji ikiwemo kuongeza Bajeti ya Dawa na Vifaa Tiba kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi bilioni 270  kwa mwaka huu wa fedha.

Ongezeko hilo limewezesha upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kufikia asilimia 89.6 kutoka asilimia 36 mwaka 2015/16. Aidha upatikanaji wa dawa muhimu umepanda kutoka wastani wa asilimia 35 tu hadi asilimia 93.

Sekta ya madini nayo, Dkt. Abbasi alisema kuwa “Serikali iliweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 1.5 kwa mwaka kutoka kwa wachimbaji wadogo wa Tanzanite pale Mirerani. Hata hivyo kabla hata ya nusu ya mwaka huu wa bajeti kufika, tayari mapato eneo la Tanzanite yamefikia shilingi milioni 788.5 sawa na asilimia 52 ya lengo la mwaka 2018/19, hii inashadidisha kuwa uamuzi wa Mhe. Rais kujenga ukuta ulikuwa makini” alisema Dkt. Abbasi

Katika miaka hii mitatu licha ya matukio ya hapa na pale, Tanzania imeendelea, kusimama kama moja ya visiwa vya amani duniani na  Taifa limeendelee kushikamana kawa kuishi kwa amani na upendo.

Aidha, Dkt, Abbasi  alisema kuwa Rais Magufuli anasimamia misingi na Watanzania leo wako huru  kuamua mambo yao kama Taifa, huku akisisitiza  kuwa safari ya kujitegemea imeanza  na mataifa mbalimbali duniani  yanafahamu   azma ya Rais Magufuli kwa Taifa lake.

JWTZ Kuwa Mwenyeji Wa Mazoezi Ya Majeshi Ya Nchi Za Jumuiya Ya Afrika Mashariki Mkoani Tanga

Jeshi  la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanatarajia kuwa wenyeji wa zoezi la mafunzo yaitwayo Ushirikiano imara 2018 litakaloshirikisha nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda ambapo mafunzo yataendeshwa mkoani Tanga .

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkuu wa Mafunzo na Operesheni  (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga amesema kuwa, zoezi hilo ni la medani na litafanyika katika wilaya za mijini pamoja na Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Ameeleza kuwa zoezi hilo litaanza rasmi tarehe 05 mpaka 21, sambamba na hilo mafunzo hayo yatalenga kujenga uwezo wa kukabiliana na uharifu pamoja na majanga.

Pia amesema kuwa dhumuni la zoezi hilo kikanda ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji, kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi zingine za kiraia ambazo zitashiriki zoezi hilo.

Sanjari na hilo kutakuwa na kazi za kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali zikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika Shule ya msingi ya Machemba iliyopo Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, pia kutakuwa na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi katika eneo la zoezi.

Hivyo, Meja Fabian ametoa rai kwa wakazi wa Tanga kuonyesha ukarimu pamoja na amani baina ya wageni watakaokua kwa kipindi chote cha mafunzo kama walivoonyesha mwaka jana ambapo mafunzo yalikua yakiendeshwa.

TTCL Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Kupunguza Wafanyakazi 550


 

Wafanyakazi Watano Wa NEMC Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma Za Kughushi Saini Ya Waziri Januari Makamba

Wafanyakazi watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi, ikiwamo kula njama na kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Januari Makamba.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka hayo jana Jumatano Oktoba 31, 2018 na wakili wa Serikali, Faraja Nguka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.

Akisoma mashtaka hayo, Nguka alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwamo la kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kusababisha hasara ya Sh 160 milioni.

Wakati washtakiwa hao wakisomewa mashtaka hayo,  mshtakiwa mwenzao, ofisa mazingira wa Nemc, Magori Wambura (38) ambaye hakuwepo mahakamani, imetolewa hati ya kumkamata ili asomewe mashtaka yanayowakabili wenzake.

Washtakiwa waliosomewa mashtaka ni ofisa mazingira wa Nemc, Deusdith Katwale (38) mkazi wa Ubungo Msewe, mtaalam wa Tehama, Luciana Lawi (33) mkazi wa Ubungo Msewe, sekretari wa baraza hilo, Edna Lutanjuka (51) mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) mkazi wa Ukonga Mombasa na ofisa mazingira NEMC, Lilian Laizer (27) mkazi wa Ukonga Mombasa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa  kati ya Septemba  27, 2016 na April Mosi, 2018 Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa kuwa  Oktoba 17, 2017 Dar es Salaam kwa udanganyifu walighushi cheti cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 wakijaribu kuonyesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na Nemc wakati wakijua si kweli.

Katika shtaka la tatu wanadaiwa kuwa Oktoba, 2017 Dar es Salaam kwa nia ovu walighushi saini ya Makamba katika cheti cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye usajili namba EC/ EIA/3366 wakijaribu kuonyesha kuwa cheti hicho ni halali na kimetolewa na Nemc wakati wakijua si kweli.

Katika shtaka la nne,  mshtakiwa Edna anadaiwa kuwa Oktoba  2017 katika ofisi za Nemc Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujua alitoa cheti cha kughushi cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 cha Oktoba 17, 2017 kwa Deogratius Chacha, akijaribu kuonyesha kuwa cheti hicho ni halali na kimetolewa na Nemc wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la tano, washtakiwa hao wote wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 27 na Aprili 6 ,2018 walijipatia kwa njia ya udanganyifu Sh160 milioni toka kwa PMM Estate (2001) Ltd kwa madai kuwa wangeweza kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira na kumpatia cheti ambacho kinatolewa na Nemc kitendo ambacho si kweli.

Katika shtaka la sita washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Septemba27, 2016 na Aprili 6, 2018 Dar es Salaam waliisababishia Nemc hasara ya Sh160 milioni.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mashtaka ya uhujumu uchumi Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza hadi Mahakama Kuu.

Washtakiwa wamepelekwa rumande na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14, 2018.
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top