Leo
Jumanne Novemba 6, 2018, mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea
ameuliza kama Serikali haioni kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa sasa hakuna
umuhimu tena kwani umekuwa ukisababisha mambo mengi ikiwemo magonjwa ya
zinaa ikiwamo HIV.
Akiuliza
swali katika kikao cha kwanza, mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea
jijini Dodoma, Mtolea alielekeza swali hilo kwa Waziri Mkuu kuwa kama
Mwalimu Nyerere alisema anawasha mwenge ili uwekwe juu ya mlima
Kilimanjaro kwanini serikali inaendelea kuutembeza.
Akijibu
swali hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi Kazi, Vijana,
Ajira na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde amesema "kuwa lengo la
mwenge ni kujenga misingi ya binadamu na utu wa mtanzania, pia umelenga
kuhamasisha ukombozi wa bara la Afrika, kupitia utaratibu huu, mwenge ni
chombo muhimu kwa kuimarisha nchi yetu.”
Mara
baada ya majibu hayo Mbunge huyo wa jimbo la Temeke alidai mwenge huo
kwa sasa unapokelewa na baadhi ya watumishi wa serikali, wakiwemo
madiwani pamoja wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari pekee akidai
kuwa wananchi wamechoshwa kuuona kila mwaka.
Kufuatia
swali hilo la Nyongeza Spika Ndugai aliamua kumkatisha mbunge huyo wa
Temeke kwa kile alichokisema kuwa swali lake halikuwa la msingi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )