Mwenyekiti
wa Chadema-Taifa Freeman Mbowe amesema, Edward Lowassa, aliyekuwa
mgombea wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa
mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hakutoa hata senti moja
alipojiunga na chama hicho.
Mbowe amezungumza hayo kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema linaloendelea hivi sasa Jijini Mwanza.
Amesema
kuwa, pamoja na kuwepo kwa kauli nyingi kwamba, Lowassa alimwaga pesa
kabla ya kujiunga na chama hicho, ukweli unabaki kuwa hakutoa pesa
yoyote kama ilivyokuwa ikidaiwa.
“Watoto wangu walikuwa wanakula sana maharage, sasa siku moja wakala nyama, jirani akasema umeona Lowassa kaja Chadema,”amesema Mbowe.
Akizungumzia
migogoro ya kichama iliyokuwa imejitokeza kwenye uchaguzi uliopita
Oktoba 25 mwaka huu Mbowe amesema, kuna kila sababu kushughulikia
migogoro hiyo kwa haraka.
“Migogoro mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama, hivyo itashugulikiwa kwa haraka,” amesema na kuongeza;“Uchaguzi mkuu wa chama ni Oktoba 2018.”
Amewaeleza
wajumbe wa mkutano huo kwamba, harakati za kisiasa hasa kukikuza chama
ni gharama kubwa, jambo ambalo chama kinajitahidi kukabiliana nalo.
Amesema kwamba, pamoja na mambo yote ndani ya chama hicho lakini suala la rushwa haliwezi kuvumiliwa hata mara moja.
Akifafanua
kauli hiyo amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeishi kwa kulea rushwa
na kwamba, hali hiyo ndio imekifikisha hapo kilipo sasa.
Amesema,
hali hiyo inaelekea kuingia Chadema jambo ambalo linaweza kusababisha
kupasuka kwa chama hicho endapo halitashughulikiwa.
“Jambo
ambalo hatutalivumilia ndani ya Chadema ni swala la rushwa kwani rushwa
inagawa taifa, sasa swala la rushwa lililelewa na CCM na sasa inataka
kuingia Chadema,” amesema.
“Kuna
majimbo kama Iringa, Rukwa, Arusha Chadema waliachiwa kwa asilimia mia
moja na Ukawa lakini kwanini wameshindwa kuchukua ushindi wa kutosha
katika majimbo hayo?” amehoji.
Akizungumzia changamoto za Ukawa, Mbowe amekiri kuwepo na kwamba hakuna sababu ya kuzikwepa.
“Changamoto zilizopo ndani ya Ukawa hakuna haja ya kuzikimbia bali ni kupambana nazo,” amesema.
Akizungumzia
umoja wa kitaifa amesema kwamba Chadema hakikubaliani na mtu yoyote
anayetaka ama kushabikia kauli za kuligawa taifa.
“Nawashauri
tunapokuwa popote lazima tukatae nchi yetu kugawanyika vipande vipande.
Hatukotayari kufanya kosa kama hilo wala kushabikia kuligawa taifa ,” amesema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )