Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) inatoa siku 60 kuanzia tarehe 14 Machi, 2016 kwa wanufaika
wote wa mikopo wanaodaiwa na HESLB kujitokeza na kuanza kulipa madeni
yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, katika muda huu wa siku 60
waajiri pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa
kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo
vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Taarifa zinazopaswa kuwasilishwa
zijumuishe majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.
Itakumbukwa kuwa Sheria iliyoanzisha
HESLB (Sura 178) (kama ilivyorekebishwa) inatoa wajibu kwa mnufaika wa
mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.
Wajibu wa Mwajiri
Hivyo basi, taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao bado hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe. Adhabu ya kutotekeleza wajibu huu kwa mwajiri ni faini ya shilingi milioni saba (Tshs milioni 7) au kifungo au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, baada ya
HESLB kupokea orodha kutoka kwa mwajiri, itafanya uchambuzi ili kubaini
wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na kumwelekeza mwajiri kuingiza
makato ya marejesho kwenye mshahara wa mnufaika na kuwasilisha makato
hayo kwa HESLB. Adhabu ya kutowasilisha makato kwa HESLB ni faini ya
asilimia 10 ya makato yote ambayo hayajawasilishwa na faini hii inapaswa
kulipwa na mwajiri.
Wajibu wa mnufaika wa mkopo na wazazi, walezi, wadhamini
Aidha, pamoja na wajibu wa mwajiri kama ulivyofafanuliwa hapo juu, wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu tangu mwaka 1994, wana wajibu wa kisheria (Kifungu cha 19 cha sheria ya HESLB), pamoja na mambo mengine, kuitaarifu HESLB kwa maandishi mahali alipo na kuandaa utaratibu wa kulipa deni lake la mkopo wa elimu ya juu.

Iwapo mnufaika wa mkopo atashindwa kutoa taarifa hizo, adhabu yake ni kushitakiwa mahakamani.
Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha
wazazi, walezi na wadhamini wa wanafunzi walionufaika na mikopo kuwa
wana wajibu wa kisheria (chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya HESLB) wa
kuhakikisha kuwa taarifa muhimu za mnufaika waliyemdhamini zinaifikia
HESLB.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, taarifa
hizo ni pamoja na mahali alipo mnufaika, majina aliyotumia wakati
akipata mkopo, mwajiri wake na kuhakikisha mnufaika aliyemdhamini
anarejesha mkopo wake kwa HESLB.
Iwapo mwajiri, mnufaika au mdau yeyote
ana swali, awasiliane na HESLB kwa simu zifuatazo: 0754 373481; 0763 459
165 au 022 2772432/33.
Lengo la HESLB ni kuhahakisha madeni
yote yanakusaanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi
zaidi. Ili kutekeleza hili, wanufaika, waajiri na wadau wengine wote
wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kisheria ili HESLB itekeleze majukumu
yake kama ilivyokusudiwa wakati ilipoanzishwa mwaka 2004.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na
9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na
majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa
katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai
na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya
juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )