Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop na
mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema huu sio wakati wa
wasanii kuendelea kulalamika kwamba nyimbo zao hazichezwi kwenye vituo
vya radio.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni,
Sugu amesema kutanuka kwa teknolojia kumewapa wasanii uwanja mpana wa
kusambaza kazi zao bila kutegemea kituo kimoja cha radio.
“Unajua zamani kulikuwa kuna vituo vichache vya radio alafu kati ya hivyo kimoja ndo kimekamata zaidi, lakini sasa hivi radio zipo kila mahali, mitandao ya kijamii. Kwa hiyo kuna media nyingi sana, yaani kuna namna nyingi za kufikisha muziki wako kwa jamii. Kwa hiyo ni kujitia unyongo wewe mwenyewe kung’ang’ana kwamba fulani hapigi nyimbo zako,” alisema Sugu.
Aliongeza, “Kwa mfano mimi sasa hivi, ukiniuliza sijui vipi nani atapigia wimbo nani hapigi, nitajibu mimi sijali nani hapigi nani anapiga kwa sababu tutasambaziana na washikaji kwenye mitandao. Kwa hiyo wasanii ambao bado wanazilalamikia radio wabadili mitazamo yao ya kibiashara, dunia haipo huko sasa hivi. Kwanza wasanii ndio wana nguvu ya kutokumpa nguvu mmiliki wa radio, kwa mfano kama hilo tatizo lipo watu waungane sasa, waseme na sisi kuanzia leo, ni marufuku kucheza nyimbo zetu, hiyo radio itaendeshwajwe?, kwa hiyo huu sio wakati wa kulalamika,”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )