Staa wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ambaye pia ni mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or, ameripotiwa kuandaa dola milioni 40 kwa ajili ya kufanya uwekezaji mkubwa wa biashara binafsi nje ya soka.
Ronaldo anaripotiwa
kutumia zaidi ya dola milioni 40 ambazo ni zaidi ya bilioni 80 za
kitanzania kwa ajili ya kuanzisha mradi wa hoteli, ambazo zitajengwa
katika miji ya New York, Lisbon, Madeira Funchal na Madrid kwa kushirikiana ubia na Pestana Hotels, mpango huo wa Ronaldo umeandikwa na Forbes.
Ronaldo na DionĂsio Pestana ambaye ni mshirika mwenzake katika biashara
hiyo, wote wamezaliwa na kukulia Maideira Ureno, hivyo hiyo ni project ambayo inahusisha watu marafiki wawili na hotel yao ya kwanza itazinduliwa weekend hii Madeira, hoteli hizo bado zitaendelea kutumia jina la kibiashara la Ronaldo CR7.

“Kazi
yangu ni kucheza soka lakini maisha siku zote hayawezi kuendelea kuwa
kama hivi, nimeamua kuingia katika mradi huu kutokana nina timu kubwa ya
watu wanaonizunguuka duniani, mimi bado kijana na nimetimiza au
nimefanikiwa katika kila kitu, hivyo naandaa maisha yangu, mwanangu na
familia yangu kwa miaka ya baadae” >>>Ronaldo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )