Jana usiku Juni 14, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Mbwana Ally Samatta alifunga goli kwenye mchezo wa hatua za awali
kuwania kucheza Europa Ligue wakati Genk ikicheza dhidi ya Buducnost
Podgorica.
Mchezo huo ulimalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 huku
Samatta akiwa amefunga bao la pili dakika ya 79 huku baada ya Neeskens
Kebano kufunga bao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati.