Zitto Kabwe ni mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo
ambaye amekuwa akiziandika headline mbalimbali kupitia uwezo wake wa
kuichambua siasa, leo September 19 2016 Zitto kupitia ukurasa wake wa
facebook ameandika ujumbe huu.
‘Kwanini
Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL? Matapeli hawa wataendelea
kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa
Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi Bilioni 300 na riba. Kiwango
Hicho Ni zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda‘ -Zitto Kabwe
‘TANESCO
wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow na
Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini
kimemkuta Rais Magufuli? Rais Kwanini hashughulikii Ufisadi huu wa
IPTL/PAP? Nini Kinamzuia Rais Kuchukua Hatua dhidi ya Wizi huu wa
Dhahiri Kwa Taifa?‘ –Zitto Kabwe
‘Tanzania Tunapata Hasara mno, Na Hizi zote Ni Fedha za Wananchi zitakazopotea‘
• ‘Watanzania
mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye “TEGETA escrow account”, Fedha
ambazo ziligaiwa Kwa Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri‘ –Zitto Kabwe
• ‘Watanzania
Mmewapa Mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa
“capacity charges” mpaka sasa – Kinyume Kabisa na Maazimio ya Bunge
yanayotaka Mitambo Husika itaifishwe‘ –Zitto Kabwe
• ‘Baada
ya Hukumu hii Watanzania tutawalipa Standard Chartered Fedha zao kwa
mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo (Kama tungelazimika Kulipa)
tungezitoa kwenye Akaunti ya Escrow – Lakini sasa tutazitoa Hazina
zikiwa ni Kodi za Watanzania‘ –Zitto Kabwe
Ushauri Wangu – Rais achukue Hatua Zifuatazo:
• Awafikishe Mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow.
• Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO (Kama ilivyoazimiwa Na Bunge).
•
Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha
Mahakamani Kwa makosa ya Utapeli, Wizi, Uhujumu Uchumi, Utakatishaji wa
Fedha nk.
•
Ahakikishe Taifa halilipi Fedha Hizi Kwa Standard Chartered. Benki
iliyotumika Kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni
tunalotakiwa kulipa.
MUHIMU: Rais AAMUE Kusimama na WATANZANIA au kusimama na “Matapeli wa TEGETA escrow“.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )