Mwenyekiti
wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya anatuhumiwa kughushi nyaraka
za Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na kuzitumia kujipatia mamilioni ya
fedha kutoka kwa wafanyabiashara mkoani Arusha.
Aidha, taarifa hizo ambazo hazijathibishwa zilizosambaa kwenye mitandao
ya kijamii zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi wa CCM na serikali mkoani
Arusha walikuwa wakifahamu kitendo hicho lakini wakakifumbia macho.
Huu hapa chini ni ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukielezea jinsi mwenyekiti huyo alivyokuwa akifanya mambo yake.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Arusha anadaiwa kufanya
utapeli na kujipatia mamilioni ya shilingi kwa kugushi nyaraka za
usalama wa taifa na kujitambulisha kuwa ni afisa wa idara hiyo nyeti.
Taarifa kutoka vyazo vya kuaminika, inaeleza kuwa Sabaya amekuwa
akijitambulisha kuwa ni afisa wa usalama wa taifa na kutumia nafasi hiyo
kutapeli wafanyabiashara mbalimbali hasa wamiliki wa hotelini na
wengine akiwahaidi kuwatafutia kazi katika ofisi nyeti za umma.
Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni diwani wa kata ya Samabashi wilaya ya
Arumeru, kupitia chama cha mapindizi (CCM), anadaiwa kutumia nafasi ya
kughushi ya usalama wa taifa kufanya utapeli, kwa kulindwa na baadhi ya
vigogo wa CCM mkoani humo.
Baadhi ya vigogo wanaodaiwa kufahamu utapeli wa Sabaya na kuufumbia
macho ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Arusha, Catherine Magige,
na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia chama cha mapinduzi jimbo la
Arusha mjini Philemon Mollel. Wapo pia viongozi wakuu wa serikali na
baadhi ya watumishi wa umma wanaodaiwa kumficha Sabaya. Inadaiwa pia
kuwa sababu ya kugoma kuondoka ofisini kwa aliyekua Katibu wa UVCCM mkoa
wa Arusha Ezekiel Mollel ilikua ni kumlinda Sabaya.
Mmoja wa viongozi wa UVCCM wilaya ya Arusha mjini asiyekubaliana na
utapeli wa Sabaya amesema “huyu ndugu anatumia nafasi yake vibaya lakini
analindwa na wakubwa. Ameghushi kitambulisho cha usalama wa taifa
wakati yeye si mtumishi wa idara hiyo, na anatumia kitambulisho hicho
kufanya utapeli lakini hakamatwi na viongozi wanajua.
Katika tukio moja Sabaya anadaiwa kutumia kitambulisho cha idara ya
usalama wa taifa kumtapeli binti mmoja mjini Arusha kiasi cha shilingi
milioni 7 kwa ahadi ya kumpatia kazi katika migodi ya Tanzanite iliyopo
Mererani Arusha. Licha ya kutapeliwa kiasi hicho cha fedha binti huyo
pia aliombwa rushwa ya ngono japo alikataa.
Katika kisa kingine ndugu Sabaya anadaiwa kulala hoteli moja jijini
Arusha ijulikanayo kama “Sky Way Hotel” kwa muda wa siku 6 lakini
akakataa kulipa. Alipoulizwa alidai yeye ni afisa wa idara ya usalama wa
taifa hivyo hawezi kulipa.
Uongozi wa hoteli hiyo ulimzuia kutoka hadi akamilishe kulipa deni hilo
lakini Sabaya aliendelea kusisitiza kuwa yeye ni Afisa usalama wa taifa
hivyo hatakiwi kulipa. Pia aliutishia kwamba wakiendelea kumsumbua
ataifunga au kuwanyang’anya leseni ya kuendesha hoteli hiyo.
Hata hivyo uongozi wa hoteli hiyo haukutishwa na kuamua kumsachi ambapo
walikuta hana fedha taslimu lakini walifanikiwa kumnyang’anya
vitambulisho vyote na kadi za benki. Kisha wakamfungulia kesi katika
kituo cha polisi kati yenye jalada AR\RB5044\2016 ambapo pia
waliwasilisha vitambulisho vyake walivyomnyang’anya.
Baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Mwenyekiti huyo alienda kujisalimisha
polisi na kulipa deni alilokua anadaiwa na hoteli hiyo kiasi cha
shilingi 309,400 na polisi wakamkabidhi vitambulisho vyake. Jambo la
ajabu ni kwamba polisi walimrudishia hadi kitambulisho cha kughushi cha
usalama wa taifa anachokitumia kutapeli.
Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mtui
alisema Mwenyekiti huyo hana makazi rasmi na amekua mtu wa kulala nyumba
za wageni, na kufanya starehe kwa pesa anazopewa na vigogo wa CCM na
serikali ambao wamekua wakimtumia kuchafua baadhi ya viongozi wa
serikali na makada wengine ndani ya CCM”
Uchunguzi uliofanywa imebaini kuwa katika kituo cha polisi kati, Sabaya
amewahi kufunguliwa kesi 4 na watu tofauti kwa madai ya kujipatia fedha
kwa njia ya udanganyifu lakini hakuna hata kesi moja aliyopelekwa
mahakamani.
Baadhi ya viongozi ndani ya CCM mkoa wa Arusha wanajitahidi kuzima
habari kuhusiana na utapeli wa Sabaya kwa lengo la kumtumia kujinufaisha
kisiasa. Viongozi hao wamesikika mara kadhaa wakipendekeza Sabaya
kugombea uenyekiti wa UVCCM taifa licha ya tuhuma lukuki zinazomkabili.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )