Gavana
wa benki kuu, Prof. Benno Ndulu wakati akielezea taarifa ya hali ya
kiuchumi nchini amesema thamani ya Shilingi imeendelea kuwa tulivu
katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, kufuatia hatua mbalimbali za sera
ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi
kwenye uchumi pamoja na mwenendo wa uchumi ndani na nje ya nchi.
Prof.
Ndulu amesema thamani ya shilingi itaendelea kuimarika kutokana na
kuimarika kwa sekta ya nje kulikotokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa
na huduma nje ya nchi. Aidha ameongeza kuwa kupungua kwa thamani ya
bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kumechangia katika utulivu wa thamani ya
shilingi.
>>>’Kwenye upande wa thamani ya shilingi huko pia sasa karibu mwaka mzima, shilingi ya Tanzania iko stable
na kwa siku za karibuni imeimarika kidogo na matarajio yetu shilingi
itabakia kuwa stable kwasababu ukuaji wa mauzo ya nje bado umeendelea
kuwa mzuri katika nusu mwaka ya kwanza mauzo ya bidhaa za huduma nje ya
nchi yameendelea kukua mpaka kufikia asilimia 14.2.’;-Prof. Ndulu
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )