Featured
Loading...

Lulu Diva Amdhalilisha Tiffah Wa Diamond


lulu-diva-1 Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.
Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kumdhalilisha mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’ kwa kumuita mbwa wake jina Shikiki, ambalo pia ni jina jingine la utani la mtoto huyo.
Tiffah wa DMtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mrembo huyo amemuita mbwa wake huyo jina hilo, kitu ambacho kimetafsiriwa na wengi kama ni kumdhalilisha mtoto huyo wa staa mkubwa Bongo.
lulu-diva-2
Lulu Diva akiwa katika pozi.
“Jamani Diva anatafuta matatizo makubwa na D i a m o n d , kwanini kampa mbwa wake jina kama hilo ambalo pia huwa linatumiwa na Tiffah? Ana hatari sana,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilipomtafuta Lulu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, alisema ni kweli mbwa wake anaitwa Shikiki lakini hakuwa akijua kwamba mtoto wa Diamond, jina lake lingine ni hilo.
“Jamani mimi sikuwa najua kabisa kama Tiffah, jina lake lingine ni hilo, mimi nilimpa tu kama watu w e n g i n e wanavyowapa m a j i n a mbwa wao,” alisema Diva.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top