Septemba 18 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mashabiki wa soka wengi wao walijitokeza kushangilia wawakilishi pekee wa Tanzania katika soka la wanaume Serengeti Boys katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2017 Madagascar.
Serengeti Boys ambao walikuwa na sapoti kubwa ya mashabiki na sapoti ya waziri Nape Nnauye waliwakaribisha Congo Brazzaville katika mchezo wao wa kwanza wa mtoano, kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo Congo Brazzaville, kwa upande wa wanaume Serengeti Boys ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Serengeti Boys ambao
walionekana kujiamini zaidi ya wapinzani wao kutokana na kuwa nyumbani,
wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-2, magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Yohana Mkomola aliyefunga mawili na Issa Makamba, wakati magoli ya Congo yalifungwa na Langa Percy kwa mkwaju wa penati na Bopoumela Chardon.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )