MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA....
“Meneja hizo pesa nitoe za benki au zako binafsi?”
“Toa za benki mtu akikuuliza, muambia aje kwangu”
Bwana
Turma akiwa anasubiria zoezi la kufungiliwa akauti, gafla milio mingi
ya risasi ikaanza kusikika ikitokea nje na kuanza kuwachanganya bwana
Turma na muhasibu wake
ENDELEA......
Kitendo
cha wasichana, makatili kuiingilia bank ya CNB, na kuwazalilisha
wananchi walio kuwemo ndani ya benki kwa kuwatoa nje uchi kinazidi
kuiumiza serrikali.Isitoshe inamuwia ugumu Bwana Turma, na akashikiliwa
na jeshi la polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano maalumu kwani gari
lake la thamani, limehusika katika matumizi ya uvamizi wa Benki.
Dickson anatoa nje ya kibanda chake, huku akiwa na wasiwasi mwingi akiwatazama askari wawili wanaokuja kwenye kibanda chake
“Habari yako kaka?”
Askari mmoja alimsalimia Dickson
“Salama tuu mambo vipi?”
Dickson
alizungumza kwa kujikaza tuu, kuuficha wasiwasi wake kwa maana msichana
ambaye ni Rahab aliye muacha ndani anaonekana hana masihara kabisa
katika matumizi ya silaha
“Hukuona, msichana aliye vaa akipita katika maeneo haya?”
“Ahaaa
kusema kweli, sijamuona kwa maana hizi bunduki kwa jinsi zilivyokuwa
zikinguruma huko nje sikudhubutu hata kuitoa miguu yangu”
Askari wakamtzama kwa umakini Dickson, ambaye anazungumza kwa kubabaika
“ Basi tunakuomba ufunge duka lako”
“Sawa”
Askari wakaanza kuondoka na kurudi katika eneo walipo wazao, Dickson akarudi ndani huku jasho jingi lkimwagika mithili ya maji.
“Waameniambia nifunge”
Dickson alimsemesha Rahab ambaye kichwa chake amekiinamisha kwenye ukuta huku sura yake ikitazama juu.
“Dada, dada.Wamesema nifunge duka langu”
Rahab hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya, huku akimtazama Dickson jinsi sura yake inavyo mwaga jasho jingi
“Powa”
Rahab alijibu kwa kifupi, na kuzidi kumchanganya Dickson
“U...takaa humu ndani?”
“Ndio wewe funga”
“Mmmm”
Dickson
akabaki akiwa anashangaa shangaa, Rahab akainyanyua bastola yake na
kumuwekea Dickson ya kichwa, mwili mzima wa Dickson ukawa kama umepigwa
na shoti ya umeme, taratibu suruali yake ikaanza kutengeneza mchoro
sehemua ya zipu, kwani woga umemfanya hadi ameshindwa kuzuia haja ndogo
“Huwa sipendi, nizungumze mara mbili mbili.Potea”
Rahab
alizungumza huku sura yake akiwa ameikunja, na anaonekana kuwa na
hasira kali.Kwa hahara Dickson akatoka nje ya kibanda chake, na kuaanza
kufunga geti la kaduka kake hata baiskeli anazo zitengeneza hakukumbuka
kuziingiza ndani.Kwa kuchanganyikiwa akajikuta akitembea asijue ni wapi
anaelekea
Wote wanne wakiwa na bunduki zao mikononi, wakawa wanaitazama njia ambayo ni yakuingilia kwenye eneo lao la handaki.
“Tutawanyike wawili wawili”
Fetty
alizungumza huku akiikoki bunduki yake, Anna akamfwata Fetty huku
Halima na Agnes wakiwa wamesimama sehemu moja.Wakatazamana kwa muda
pasipo mtu yoyote kuzungumza neno , kisha wakaanza kukimbia mtuni,
wakiwa wameganawana kila watu wawili sehemu yao.Fetty na Anna walielekea
magharibi mwa msitu wao, huku Agnes na Halima wakielekea Mashariki mwa
msitu wao.
Askari
wakiongozwa na mbwa wao, walio fundishwa mafunzo maalumu ya kunusa kila
sehemu ambayo amepita mtu ambaye askari wanamuhitaji, ndivyo walizidi
kuendelea kuingia msituni wakiwa na bunduki zao.Huku kila mmoja akiwa na
hasira kali juu, ya maauaji yaliyo tokea siku chache zilizo pita juu ya
wezao walio uwawa kwenye kituo cha gesi kwa mlipuko mkali.Amri mmoja
iliyo tolewa na mkuu wa jeshi la polisi Bwana Gudluck Nyangoi ni kwamba
wahakikishe wanawatia nguvuni ili wahukumiwe kifungo kikali kitakacho
ishangaza dunia
Askari
wakiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Ngurumo, wanaendelea
kuuzingira msitu huku wakiwa na imani ya kufanikiwa na abushi yao wanayo
kwenda kuifanya kwenye msitu unao sadikika ndipo walipo ingia majambazi
kipindi wakitokea kufanya tukioa benki, na maelezo haya yalitolewa na
msamaria mwema ambaye, gari lao lilisimamisha kipindi askari wa usalama
barabarani walipokuwa wakifanya uchunguzi kwa kila gari ambalo lilikuwa
likikatiza katika barabara kuu ya kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )