ILIPOISHIA
“Fanya fasta basi”
Samson
akatoka nje huku akiishika shika pua yake iliyo jaa maumivu ya kupigwa
ngumi na Rahab, Samson akaingiza baiskeli ya kwanza na kutoka nje akiwa
ameishika baiskeli ya pili akitaka kuingia ndani, gafla breki za gari
aina ya Defender yenye askari wa kikosi cha F.F.U wapatao sita wakashuka
kwenye gari kwa haraka huku wakiwa na bunduki na kunza kumfwata Samson
sehemu alipo simama
ENDELEA
“Unafanya nini hapo?”
Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya ukali na kumfanya Samson kuanza kutetemeka mwili mzima
“Husikii au?” askari aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ukali
“Ni..ninaingiza baiskeli zangu ndani”
“Wewe kama nani?”
“Mimi, ni mmiliki wa hapa, mchana nilikimbia kutokana na tukio la majambazi”
Mazungumzo, yote yanavyo endelea nje Rahab anayasikiliza kwa umakini wa hali ya juu, huku bastola yake ikiwa mkononi mwake
“Mkuu tukague ndani”
Ombi
la askari huyu mwenye alama ya ‘V’ kwenye bega moja, likamfanya Samson
kubaki akiwa anaduwaa, ila akajikaza asiuonyeshe mstuko wake kwani
hakujua kitatokea nini baada ya askari hao kuingia ndani ya duka lake na
kumkuta Rahab
“Kuna vurugu, maeneo ya Sinza kwa Remy, OVER”
Ilisikika sauti kupitia redio ya upepo aliyo ishika mkuu wao na kusababisha, kuto kulijibu ombi la asakri wake
“Tunakuja Over”
Alijibu,
huku akiiwatazama askari wake na wote kwa pamoja wakarudi kwa haraka
kwenye gari lao na kuondoka kwa kasi kubwa.Sammso akashusha pumzi
nyingi, kwa haraka akaanza kuingiza baiskeli zake zote
“Tuondoke, tayari nimesha maliza”
Samson alimuambi Rahab na wote wakatoka nje kwa umakini, huku wakichunguza kila eneo la nje.Samson akapanda kwenye baiskeli yake
“Panda twende”
Rahab akaitazama baiskeli ya Samson kwa umakini,
“Siwezi kukivunja kiti chake”
“Wewe
panda twende kwani kikivunjika tutajua mbele ya safari, isije hawa
jamaa wakarudi na kunikuta tupo pamoja hapa sijui itakuwaje”
“Mmmm!!”
Rahab
akapanda kwenye baiskeli na taratibu Samson akaanza kubadilisha gia
moja baada ya nyingine zilizopo kwenye baiskeli yake kutoka gia laini
kuelekea gia ngumu, na jinsi anavyozidi kuendesha baiskeli ndivyo mwendo
wa baiskeli yake inavyozidi kuongezeka.Ndani ya dakika kumi wakawa
wamefika nyumbani kwa Samson, wakaingia ndani kisiri pasipo mtu yoyote
kuwaona
Ukimya
ukatawala kati yao, na hakuna mtu aliye msemesha mwenzake kwa wakati
huu, alicho kifanya Rahab, akavua viatu vyake na kupanda kitandani na
kumfanya Samson kuendela kusimama akimtazama Rahab jinsi alivo jilaza
chali akitazama paa la chumba chake
“Panda ulale”
Rahab alizungumza huku akimtazama Samson usoni
“Ahaa, mimi nitalala hapa chini”
“Wewe vipi, kinacho kuogopesha wewe ni nini?”
“Siogopi”
“Sasa kinacho kubabaisha ni nini, hebu acha ufala panda kitandani kwako ulale, ila onyo lala usiniguse mwili wangu”
“Mmmmm”
“Guna, tu”
“Ndio maana ninakuambia kwamba nitalala hapa chini”
“Sijawai kuona dume zima likiwa linaogopa kulala na mwanamke kitanda kimoja”
Samson
akamtazama Rahab kwa umakini kisha akapanda juu ya kitanda na kuchukua
mito miwili na kutengeneza mpaka kati yao ambao hakuna mtu ambeye
angeweza kumgusa mwengine, Samson taratibu akajikuta akiaanza kutawaliwa
na hisia za mapenzi juu ya Rahab ambaye anaonekana kawa si mtu wa
masihara hata kidogo.Samson akauingiza mkono wake mmoja chini ya mto, na
taratibu akanza kuupeleka katika eneo alilo lala Rahab.Akafanikiwa
kuufikisha mkono wake alipo lala Rahab, akamminya kwenye maeneo ya mbavu
, ila Rahab akatulia kimya na kujifanya kama amelala, Samson akarudia
tena kumminya Rahab eneo la mbavu na Rahab hakuonyesha mtikisiko wowote
“Kitu kimelinki”
Samson
alizungumza kimoyo moyo, huku usoni mwake akiachia tabasamu pana
lililojaa uchu mkali wa mapenzi, akajigeuza na kujilaza kiubavu,
taratibu mkono wake mmoja ukaanza kupandisha hadi kwenye chuchu ya
Rahab, hata kabla Samson hajaukandamiza mkono wake vizuri kwenye chuchu
ya Rahab, gafla macho yake yakakutana yakitazamana na jicho la bastola,
aliyoishika Rahab kwa umakini
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )