Featured
Loading...

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 15 & 16

MUANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA 

ILIPOISHIA
“Fanya fasta basi”
Samson akatoka nje huku akiishika shika pua yake iliyo jaa maumivu ya kupigwa ngumi na Rahab, Samson akaingiza baiskeli ya kwanza na kutoka nje akiwa ameishika baiskeli ya pili akitaka kuingia ndani, gafla breki za gari aina ya Defender yenye askari wa kikosi cha F.F.U wapatao sita wakashuka kwenye gari kwa haraka huku wakiwa na bunduki na kunza kumfwata Samson sehemu alipo simama

ENDELEA
“Unafanya nini hapo?”
Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya ukali na kumfanya Samson kuanza kutetemeka mwili mzima
“Husikii au?” askari aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ukali
 
“Ni..ninaingiza baiskeli zangu ndani”
“Wewe kama nani?”
“Mimi, ni mmiliki wa hapa, mchana nilikimbia kutokana na tukio la majambazi”
Mazungumzo, yote yanavyo endelea nje Rahab anayasikiliza kwa umakini wa hali ya juu, huku bastola yake ikiwa mkononi mwake
“Mkuu tukague ndani”
Ombi  la askari huyu mwenye alama ya ‘V’ kwenye bega moja, likamfanya Samson kubaki akiwa anaduwaa, ila akajikaza asiuonyeshe mstuko wake kwani hakujua kitatokea nini baada ya askari hao kuingia ndani ya duka lake na kumkuta Rahab
“Kuna vurugu, maeneo ya Sinza kwa Remy, OVER”
Ilisikika sauti kupitia redio ya upepo aliyo ishika mkuu wao na kusababisha, kuto kulijibu ombi la asakri wake
“Tunakuja Over”
 
Alijibu, huku akiiwatazama askari wake na wote kwa pamoja wakarudi kwa haraka kwenye gari lao na kuondoka kwa kasi kubwa.Sammso akashusha pumzi nyingi, kwa haraka akaanza kuingiza baiskeli zake zote
“Tuondoke, tayari nimesha maliza”
Samson alimuambi Rahab na wote wakatoka nje kwa umakini, huku wakichunguza kila eneo la nje.Samson akapanda kwenye baiskeli yake
“Panda twende”
Rahab akaitazama baiskeli ya Samson kwa umakini,
“Siwezi kukivunja kiti chake”
“Wewe panda twende kwani kikivunjika tutajua mbele ya safari, isije hawa jamaa wakarudi na kunikuta tupo pamoja hapa sijui itakuwaje”
“Mmmm!!”
 
Rahab akapanda kwenye baiskeli na taratibu Samson akaanza kubadilisha gia moja baada ya nyingine zilizopo kwenye baiskeli yake kutoka gia laini kuelekea gia ngumu, na jinsi anavyozidi kuendesha baiskeli ndivyo mwendo wa baiskeli yake inavyozidi kuongezeka.Ndani ya dakika kumi wakawa wamefika nyumbani kwa Samson, wakaingia ndani kisiri pasipo mtu yoyote kuwaona
 
Ukimya ukatawala kati yao, na hakuna mtu aliye msemesha mwenzake kwa wakati huu, alicho kifanya Rahab, akavua viatu vyake na kupanda kitandani na kumfanya Samson kuendela kusimama akimtazama Rahab jinsi alivo jilaza chali akitazama paa la chumba chake
 
“Panda ulale”
Rahab alizungumza huku akimtazama Samson usoni
“Ahaa, mimi nitalala hapa chini”
“Wewe vipi, kinacho kuogopesha wewe ni nini?”
“Siogopi”
“Sasa kinacho kubabaisha ni nini, hebu acha ufala panda kitandani kwako ulale, ila onyo lala usiniguse mwili wangu”
“Mmmmm”
“Guna, tu”
“Ndio maana ninakuambia kwamba nitalala hapa chini”
“Sijawai kuona dume zima likiwa linaogopa kulala na mwanamke kitanda kimoja”
 
Samson akamtazama Rahab kwa umakini kisha akapanda juu ya kitanda na kuchukua mito miwili na kutengeneza mpaka kati yao ambao hakuna mtu ambeye angeweza kumgusa mwengine, Samson taratibu akajikuta akiaanza kutawaliwa na hisia za mapenzi juu ya Rahab ambaye anaonekana kawa si mtu wa masihara hata kidogo.Samson akauingiza mkono wake mmoja chini ya mto, na taratibu akanza kuupeleka katika eneo alilo lala Rahab.Akafanikiwa kuufikisha mkono wake alipo lala Rahab, akamminya kwenye maeneo ya mbavu , ila Rahab akatulia kimya na kujifanya kama amelala, Samson akarudia tena kumminya Rahab eneo la mbavu na Rahab hakuonyesha mtikisiko wowote
 
“Kitu kimelinki”
Samson alizungumza kimoyo moyo, huku usoni mwake akiachia tabasamu pana lililojaa uchu mkali wa mapenzi, akajigeuza na kujilaza kiubavu, taratibu mkono wake mmoja ukaanza kupandisha hadi kwenye chuchu ya Rahab, hata kabla Samson hajaukandamiza mkono wake vizuri kwenye chuchu ya Rahab, gafla macho yake yakakutana yakitazamana na jicho la bastola, aliyoishika Rahab kwa umakini
                                                                                           **************
Vyomo vingi vya habari ndani na nje ya nchi ya Tanzania vimepambwa na taarifa juu ya kukamatwa kwa majambazi sugu walio walaza askari wengi macho kwa kazi moja ya kuwatafuta popote walipo, usiku na mchana.Sura za Fetty, Anna, Halima na Agnes zimepamba magazeti mengi ikiwemo hata magazeti ya udaku,askari walio fanikisha kukamatwa kwa majambazi hawa, ikawa ni moja ya ofa kubwa katika maisha yao kwa kila mmoja kupandishwa cheo kimoja kutoka sehemu alipo hadi sehemu ambayo mkuu wa majeshi Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania alihisi inastahili kwao.

Japo kuna misiba mingi ya askari walio kufa katika oparesheni kimbunga ya kuwavamia majambazi hao, familia za askari walio kufa zikapewa kiasi cha shilingi milioni mia moja, pamoja na bima za matibabu kwa wale askari wote walio na tattoo chini ya umri wa miaka kumi na nane
 
Ila haikuwa furaha kwa dokta Wiliam ambaye yupo nchini mwao kwa ajili ya likizo ya muda mrefu, jambo ambalo linazidi kumuumiza kichwa ni kuhusu mahali alipo jificha Rahab kwani hakuwepo katika orodha ya walio kamatwa, akaitoa simu yake ya mkononi na kuingiza namba za rais wa Tanzania, kabla hajapiga akaanza kujiuliza mswali yasiyo na majibu kichwani mwake
 
“Nikimpigia ninamuambia nini, je akiniuliza ilikuwaje nikawaagiza kwenye tukio hilo walilo lifanya itakuwaje?”
Dokta William alijiuliza swali ambalo akabaki akiitazama namba ya rais, taratibu akakishusha kidole gumba cha mkono wa kulia, ulio ishika simu yake na kuiminya batani yenye alama ya kijani, inayo ashiria kuwa ndio batani ya kupiga simu, akaiweka sikioni simu yake huku mwili ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa anameza mafumba ya mate mengi, ndani ya sekunde kadhaa sauti nyororo kutoka upande wa pili wa simu ukaanza kusikika
“MTUMIAJI WA SIMU UNAYE MPIGIA, ANAONGEA NA SIMU NYINGINE. TAFADHALI SUBIRI AU KATA SIMU NA UPIGE TENA”
 
Dokta William akakata simu yake na kushusha pumzi nyingi huku akiitazama, akaiingiza simu yake mfukoni na kunyanyuka kwenye kochi lake alilo likalia, kabla hajafanya chochote akasikia simu yake akiita, kwa haraka akaitoa na kukuta namba ya rais ikiingia, akaipokea na kuiweka simu yake sikioni
 
"Ndio muheshimiwa raisi"
"Niliona simu yako ikiingia Dokta William"
"Ndio muheshimiwa, ila nilitaka tuzungumze kuhusiana na hao mabinti walio kamatwa napolisi"
 
"Una maoni gani juu yao?"
"Hao ndio wale vijana ulio niagiza kufanya nao kazi ya kuwasaka wote, wanao isumbua serikali yako"
"Kwa hiyo mimi nifanyeje?”

"Usiwachukulie sheria kali bado tunawahitaji"
"Siwezi kufanya ujinga kama huo kwasababu wametugharimu sana serikali yetu"
Raisi alizungumza kwa hasira kisha akakata simu, na kumuacha Dokta William akibaki akiitazama simu yake pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
 
     ******
Mwili wa Samson ukaanza kutetemeka, baada ya macho yake kutazamana na bastola ya Rahab
“Nilikuambia usiniguse, mimi sio Malaya sawa?”
Rahab alizungumza kwa sauti ya ukali
“Sawa mama”
 
Samson ili kuepukana na dhahama ya kupigwa risasi na Rahab taratibu akajishusha chini, akachukua taulo lake na kulilaza sakafuni na kujilaza.Masaa yakazidi kutakika hadi asubuhi ambapo Samson akawa wa kwanza kustuka kutoka usingizini, hii ni kutokana na ubaridi mkali uliompiga kwenye sakafu, akatoka nje na moja kwa moja akakimbilia chooni kutoa haja ndogo iliyo mbana sana kisha akarudi chumbani kwake
 
Akamkuta Rahab akiwa, anajinyoosha nyoosha huku akipiga miayo, Samson akamsalimia Rahab ila hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumtazama tu.
“Simu yako ina redio?” Rahab aliuliza
“Ndio”
 
“Inashika stesheni gani?”
“TBC FM, Redio One , Clouse”
“Weka TBC”
Samson hakuwa mbishi zaidi ya kuiwasha simu yake, sehemu ya redio, wakakuta miziki ikiwa imerindima kwenye kituo hicho
“Weka stesheni nyingine”
 
Samson akatii na kuweka stesheni nyingine, hakuna stesheni iliyokua na kitu cha maana na kumfanya Rahab kujipa matumaini wenzake wapo katika hali salama.Samson akamuomba Rahab amsubirie anakwenda kuchukua kifungua kinywa
“Unakwenda kununua nini?”
“Mihogo ya kukaanga”
“Powa, chukua na gazeti”
“Gazeti la kufungia hiyo miogooo au gazeti la kusoma?”
“Wewe unaona gazeti gani?”
“Powa nimekuelewa”
 
Samson alizungumza huku akitabasamu, akatoka ndani kwake a kwenda mtaa wa pili ambapo kuna biashara za mihogo ya kukaanga, kifungua kinywa ambacho Samson anakipenda na pia kinarahisisha matumizi ya pesa yake, hii ni kutokana na kipande kimoja cha muhogo kuwa ni shilingi hamsini ya kitanzania, Samson akanunua magazeti mawili yaliyo na picha za wasichana ambao moja kwa moja akawatambua ni wale walio kuwa wakizipiga risasi kama wendawazimu.

Kwa mwendo wa haraka huku mkono wake mmoja akiwa ameshika kifuko chenye mihogo ya elfu moja na mkono wake mwingine akiwa na magazeti akafika nyumbani na kuingia ndani
 
“Oya kuna habari hapa sio nzuri”
Samson alizungumza huku akimpa gazeti, Rahab
“Habari gani?”
Rahab akachukua gazeti la Mwananchi na kuligeuza kurasa ya kwanza na kuwaona wezake wakiwa wapo chini ya ulinzi wa polisi, jasho jembamba lililo endana na mapigo ya moyo ya kasi vikaanza kuchukua nafasi kwa wakati mmoja, hakuamini kama wezake wamekamatwa, akafungua kurasa ya ndani na kushuhudia picha za wenzake wakiwa wanapandishwa kwenye magari ya polisi
 
“Inabidi tufanye kitu chochote kuweza kuwaokoa wezangu”
Rahab alizungumza huku mwili mzima ukiwa unamtetemeka
“Ufanye na nani?”
“Na wewe”
“Mimi?”
“Ndio”
“Siwezi”
Kwa haraka Rahab akasimama na kuichomoa bastola yake na kuiweka kichwani mwa Samson, huku mwili mzima ukiendela kumtetemeka kwa hasira kali, iliyomfanya kuyang’ata meno yake kwa nguvu zake zote
 

SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……16

“Basi basi, nitafanya”
Samson alizungumza kwa sauti ya kukata roho na kumfanya Rahab kumuachia, na kukaa pembeni, ukimya ukaanza kutawala kati yao, huku Samson macho yake yote yakiwa kwa Rahab aliye kaa kitandani huku amejiinamia chini
“Unaweza kutumia silaha?”
“Hapana”
Rahab akaachia msunyo mkali huku akimtazama Samson
                                                                                              *******
Mipango ya kuwapeleka Fetty na wenzake katika mahakama kuu inayoshuhulika na maswala ya kigaidi ‘THE HUNG’, ikaanza kufanyika kwa ulinzi mkali wa vikosi vyote vya ulinzi vilivyopo nchini Tanzania, tangu kukamatawa kwao maisha yao yamekuwa ni yakufungwa vitambaa vyeusi katika macho yao pamoja na kufungwa pingu ambazo ni toleo jipya na mara nyingi hutumika katika mataifa makubwa kama Marekani na Uingereza katika swala zima la kuwafunga wahalifu walio shindikana na serikali zao, wanao hesabiwa kama magaidi.
 
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali duniani wameweka kambi nje ya makao makuu ya jeshi la polisi, kila mmoja akisubiri kunasa habari ya ni siku gani magaidi hao wa kike watasafirishwa kupelekwa mahakamani, kwani kila mmoja anahamu sana ya kuwaona wasichana hao wanafananiaje kwani matukio waliyo yafanya tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru mwaka 1961, hapakutokea kundi au watu walio iumiza serikali kwa kiasi kikubwa sana katika kuua idadi kubwa ya polisi kama walivyo fanya  Fetty na wenzake
 
IGP bwana G.Nyangoi kwa mara ya kwanza anajitokeza mbela ya waandishi wa habari huku akiwa ametawaliwa na tabasamu kubwa, kwani kuwakamata magaidi hawa kwake ni jambo kubwa la kufurahisha na ni miongoni mwa ushindi mkubwa tangu akabidhiwe kiti cha kuliongoza jeshi la polisi
“Nitakaribisha, maswali yasiyo zidi matano tu, ili kuokoa muda”
 
Bwana G.Nyangoi alizungumza mbele ya waandishi wa habara walio zitega kamera zao za aina mbali mbali 
 
“Mimi ni Jonh kutoka shirika la utangazaji la BBC Swahili, Ningependa kufahamu kama jeshi la polisi ni hatua gani ambazo mmepanga kuzichukua kwa askari wote walio kufa katika harakati za kuwakamata hawa magaidi?”
 
“Nilisha zungumza hapo awali, kwa wale askari wangu wote walio fariki katika tukio zima la kuwatafuta hawa magaidi, familia zao zimelipwa kiwango cha shilingi milioni mia moja, huku wale wenye watoto wao watasomeshwa na serikali kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu”
 
“Je, magaidi hao mmepanga kuwasafirisha kwa usafiri gani?”
“Magaidi, watasafirishwa kwa kutumia ndege”
“Ndege gani?”
“Ndege za jeshi zitahusika katika kuwapeleka mahakama kuu ya magaidi”
 
“Je, kwa nini wasihukumiwe hapa hapa nchini Tanzania hamuoni, kuwapeleka huko inagharimu kiasi kikubwa cha pesa?”
 
“Kwakiwango walicho kifikia hawa mabinti  ni kikubwa sana na kimefikia kiwango cha kuhesabiwa kama magaidi wa kimataifa na sisi kama washiriki wa umoja wa mataifa tunawaachia umoja wa mataifa kufanya kazi juu ya hawa watu, Asanteni sana kwa maswali yenu”
 
“Muheshimiwa swali moja la mwisho”
“Ehee uliza, ila hili ndio litakuwa swali langu la mwisho, ninawahi kikao sawa jamani”
 
“Tumesikia kwamba mmeshirikiana na FBI katika kuwakamata hawa mabinti , nyinyi mlishindwa kufanya hiyo kazi?”
 
“Hapana, vijana wetu wenye mafunzo kamili ndio wameifanya hiyo kazi, Asanteni sana”
IGP Bwana G.Nyangoi akawaaga waandishi wa habari na kuingia zake ndani na kuwaacha wakiwa wanaulizana maswali wao kwa wao
                                                                                                ********
“Shiti…, huu ni ujinga”
Rahab alizungumza huku akiitazama Tv ndogo iliyomo kwenye chumba cha Samson, kwa kupitia chaneli ya Star Tv aliweza kuyaona mahojiano  ya waandishi wa habari na mkuu wa jeshi la polisi bwana G.Nyangoi
 
“Tutafanyaje, wakati watu ndio hao tayari wamekamatwa?”
Samson aliizungumza huku akimtazama Rahab aliye ikunja sura yake, Rahab akainyanyua sura yake na kumtazama Samson kisha akairudisha kwenye Tv inayoonyesha miziki ya bongo Flevar
“Tunaweza kuwapata”
“Tutawapataje?”
“Nitakuonyesha jinsi ya kuwapata”
                                                                                                

************
Rahab anafanikiwa kufika katika uwanja wa ndege wa Julias Kambarae Nyerere, bila ya mtu yoyote kuweza kumgundua, kwa jinsi alivyo jitanda mtandio kichwani na kujipara vilivyo, haikuwa rahisi kwa mtu yoyote kuhisi kama yeye ni jambazi, kitu cha kwanza kukifanya anamtafuta Ludovirk mwanaume ambaye alishawahi kulala naye kipindi cha nyuma akiwa anafanya kazi ya kujiuza mwili wake, na Ludorvick anahusika katika kitengo cha ukaguzi.

Kwa bahati nzuri akamuona Ludorvick akiwa amesimama kwenye moja ya nguzo, huku akizungumza na simu.Kwa mwendo wa umakini Rahab akatembea hadi sehemu alipo simama Ludorvick na kumgusa bega kwa nyuma
“Ludo”
Rahab aliita kwa sauti ya uchokozi ambayo ni nyepesi sana, na iliyo legea.Ludovick akageuka na kukutana na Rahab
“Sawa ngoja nitakupigia kuna kazi ninaifanya mara moja hapa”
 
Ludorvick alimjibu mtu anaye zungunza naye kwenye simu, akaikata simu yake na kumkumbatia Rahab kwa nguvu
“Upo wewe?” Ludorvick alizungumza kwa sauti ya mshangao, na iliyo jaa furaha sana
“Ndio nipo”
“Umezidi kupendeza, mpenzi wangu”
“Asante”
 
“Twende ofisini, hapa si unaona jinsi watu walivyo wengi”
Ludorvick akaongozana na Rahab hadi ofisini kwake, huku njiani Rahab akiwatazama askari kwa umakini na hakuna ambaye anamfwatilia, wakaingia ofisini mwa Ludorvick, kitu cha kwanza alicho kifanya Ludorvick ni kuanza kuing’ang’ania midomo ya Rahab na kuanza kuinyonya kwa fujo, huku akiachia pumzi nyingi.Rahab hakutaka kujibana na akamuacha Ludorvick kufanya yake
“Mmmm, baby tupo ofisini banaa”
Rahab alizungumza kwa sauti ya kudeka
“Ngoja kwanzaa, kidogo”
 
Ludorvick alizungumza huku akiaanza kuvua koti lake la suti
“Jamani baby ngoja kwanza tuzungumze, leo nitalala na wewe usiku kucha”
“Kweli” Ludorvick alizungumza huku akihema kama bata mzinga
“Ndio baby, usijali kwa hilo”
 
Rahab alizungumza kwa sauti ya kudeka na kuzidi kumpagawisha Ludorvick, mchaga huyu anaye babaika sana kwenye swala zima la mapenzi, na kila anapovuta hisia siku aliyo pewa penzi motomoto na Rahab basi anajikuta mwili mzima ukimsisimka.

Ludorvick akaliokota koti lake la suti, alilokuwa amelitupa chini, Rahab akakaa kwenye kiti kilichopo karibu na meza ya Ludorvick
“Niambie mke wangu”
“Safi, tuu.Mume ninishida”
“Unashida gani mke wangu, mtoto mzuri kama wewe?”
“Mmmm, kuna shida nahitaji unisaidie”
“Zungumza, kama ni pesa wewe niambie tu nitakupa kiasi chocote utakacho kihitaji”
 
Kabla Rahab hajazungumza kitu simu ya mezani mwa Ludorvick ikaita na kumfanya Ludorvick kuachia msonyo mkali na kuipoke na kuminya kitufe cha kuifanya sauti kuwa kubwa(Luodspeker)
 
“Ludorvick andaa ndege yangu, ninasafari saa mbili na nusu usiku, hakikisha inakaguliwa vya kutosha”
Sauti nzito ilizungumza kutoka upande wa pili wa simu
“Sawa sawa, mheshimiwa Raisi”
Simu ikakatwa na Ludorvick akabaki akiwa ameduwaa kwani hakutegemea kupokea simu ya Raisi kwa wakati kama huu,
“Nani?’
“Raisi”
“Mmmmm”
“Yaani hapa amesha nivunja nguvu mke wangu?”
“Kwa nini?’
“Ndio nilikuwa ninataka kutoka kazini, hapa itanibidi nikasimamie zoezi zima la ndege yake kukaguliwa , hadi aondoke nchini na sijui anakwenda wapi”

“Twende nikakusaidie mpenzi wangu, uku unafanya kazi ninakupeti peti”
“Eti eheee”
 
“Ehee, kwani sipaswi kuwa karibu nawe?”
“Unapaswa, ngoja niwapigie simu wakaguzi wangu”
Ludorvick akawapigia simu wakaguzi wake wanaohusika katika ukaguzi wa ndege na kuwapa kazi hiyo na kuwaamuru waanze mara moja pasipo kupoteza muda.

Ludorvick akatoka na Rahab hadi sehemu ya maegesho ya ndege ya Rais na kuwakuta watu wake  akiwa katika kazi ya ukaguzi wa ndege ya Rais  Praygod Makuya, ambayo ni aina ya ‘Air Force’ aliyopewa na serikali ya Marekani, katika kuimarisha ulinzi katika safari zote za raisi wa Tanzania
 
“Kumbe Raisi anandege kubwa kama hii?”
“Ndio, hii Raisi alipewa kama msaada, si unajua Marekani na TANZANIA tunashirikiana katika mambo mengi”
“Ahaaaa, kwa hiyo humo ndani anaingia Raisi peke yake au?”
“Humo anaingia Raisi na wajumbe wake wote”
“Ahaaa”
 
“Twende ukaone ndani”
Ludorvick alizungumza huku akiongozana na Rahab kupandisha ngazi ndefu kuelekea juu ulipo mlango wa kuingilia ndani kwenye ndege kubwa, ambayo ukiachilia ukubwa na ubora wa ndege anayo tembelea Raisi wa marekani, inayo fwata ni ndege hii anayo tembelea Raisi wa Tanzania Dokta Praygod Makuya.

Macho ya Rahab yakawa na kazi ya kutazama sehemu zote za ndani ya ndege
“Hii ndege, wamarekanai wameweza kutengeneza, kwa maana inavitu vingi sana vya kumlinda Raisi”
“Ahaaaa, natamani niipande na mimi kuwa miongoni mwa abiria”
 
“Ahaaa hii huwezi kupanda, ukiachilia ikulu ya raisi, akiwa hewani Raisi Ikulu yake inakuwa humu ndani na ndani ya hiyo ofisi anaweza kufanya kazi zake zote kama akiwa ardhini”
 
Ludorvick akaendelea kumuelekeza sehemu mbali mbali za kwenye ndege hii ya kisasa ya Raisi wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania bwana Praygod Makuya.Pasipo Ludorvick kuona,
“Baby ninakuomba niingie chooni”
“Sawa ngoja mimi niingie kwenye chumba cha marubani niaangalie kama kuna usalama”
“Sawa”
 
Rahab akachukua nguo nne za wahudumu wa ndege ya Raisi na kuingia nazo chooni pasipo Ludorvick kuona tukio hilo, akazikunja vizuri na kuzificha kwenye makalio yake kisha alipo hakikisha kwamba yupo vizuri akatoka chooni na kumkuta Ludorvick akimsubiria
“Umeona hivyo vyoo vilivyo vizuri”
“Ndio, hivi wahudumu wa Raisi wanaingia saa ngapi ndani ya ndege?”
“Lisaa limoja kabla ya raisi kuingia ndani ya ndege”
Ludorvick na Rahab wakatoka kwenye ndege na kwenda sehemu ya kutokea, nje ya uwanja wa ndege kwa kupitia geti la nyuma ya uwanja
“Baby ngoja nikupe pesa, uchukue taksi mimi ngoja nirudi nikawasimamie hawa vijana”
“Sawa”
 
Ludorvick akatoa laki mbili na kumkabithi Rahab
“Alafu sijachukua namba yako ya simu”
“Sina simu mume wangu”
“Ohooo basi ngoja nikuongezee pesa ukanunue nyingine”
“Sawa nitashukuru”
Ludorvick akatoa laki na nusu na kumkabithi Rahab kisha akamtajia namba yake ya simu na Rahab akaahidi kuishika kichwani mwake
“Sawa baby nitakupigia”
Rahab akaondoka huku akiwa na furaha kubwa moyoni mwake, akachukua taksi hadi nyumbani kwa Samson na kumkuta Samson akiwa amejilaza kitandani huku akionekana kuwa na mawazo mengi
“Umetoka wapi?”
Samson alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akimtumbulia mimacho Rahab
 
“Unaniuliza wewe kama nani?”
“Sio ninakuuliza kama nani, ila nataka kujua unatatoka wapi kumbuka kwamba hapa upo kwangu?”
“Hupaswi kujua, mwehu nini wewe?”
Samson akanyanyuka kwa hasira na kumzaba Rahab kibao cha shavuni kilicho myumbisha hadi kikamuangusha chini
 
ITAENDELEA...

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top