Kutoka
kushoto ni balozi wa shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi
ya Time To Help, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza na Meneja wa
Shule za Feza mkoani Mwanza, Metin-Er.
Na BMG
Uongozi
wa Shule za Feza (Feza Schools) nchini Tanzania mwakani unatarajia
kufungua tawi la shule hizo Jijini Mwanza, ili kuendelea kufikisha
karibu upatikanaji wa elimu karibu na jamii nchini.
Balozi wa
shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi ya Time To Help
(kushoto), aliyasema hayo juzi jumatatu Septemba 12,2016 wakati wa zoezi
la kukabidhi msaada wa mboga (nyama) kwa makundi mbalimbali ya wahitaji
mkoani Mwanza kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj.
Alisema
lengo la Shule za Feza kwa kushirikiana na taasisi yake ya Time To Help
ni kusaidia jamii ya watanzania bila kujali dini, kanila wala mipaka ya
aina yoyote.
Msaada
uliotolewa na Shule za Feza ni nyama kilo 500 ambazo ziligawiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella, kwenye Kituo cha Wazee Bukumbi, Bakwata mkoani
Mwanza, Taasisi za Juqusuta, Ummy Salama na Masjid Noor Mahina.
Msaada wa mboga uliotolewa Shule za Feza mkoani Mwanza.
Shule za
Feza zinapatikana katika mataifa mbalimbali duniani ambapo nchini kuna
tawi Jijijini Dar es salaam na sasa mkakati ni kufungua tawi mkoani
Mwanza. (P.T)
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )