Featured
Loading...

Tanzania Mpya, Uongozi Makini


tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania.
Uongozi ni hali ya muhusika mmoja kuwa na dhamana, madaraka na uwezo wa kuwaongoza wengine. Ili uwepo uongozi lazima awepo kiongozi na wanao ongozwa. Kiongozi anaweza kuwa rais, waziri, mbunge, mtemi, mfalme,  mkurugenzi, chifu,  na hata muwakilishi wa wengine kama vile mwenyekiti au mjumbe wote ni viongozi.
Sifa za kiongozi bora  ni pamoja na akili timamu (ufahamu), kiongozi ni lazima awe na ufahamu dhidi ya kundi kubwa analoliongoza katika nyanja tofauti kama vile mazingira, tamaduni. Mila na desturi na hata matatizo ya ano waongoza.
Maadili mema kwa kiongozi ni sifa muhimu, maadili ya jumuisha vitu vingi ikiwemo tabia njema, ucha Mungu na uadilifu. Bila kuwa namaadili mema huwezi kuwa muadilifu hivyo maaadili ni sifa ya msingi kwa kiongozi. Bila kuwa na maadili mema kiongozi hatokubalika na jamii anayoingoza na lazima utatokea mpasuko mkubwa ambao utaigawa jamii katika matabaka.
MagufuliiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kiongozi lazima awe mwaminifu. Ili kufikia malengo kwa jamii yoyote au taasisi lazima uwepo kiongozi mwaminifu. Shabaha ama malengo hayata timia ikiwa kiongozi si mwanifu kwa watu anao waongoza. Uamini ni pamoja na kufanya yale aliyoagizwa bila upendeleo wala kuangalia maslahi ya kundi lolote ispo kuwa maslahi ya anao waongoza.
Tanzania kwa awamu zote zilizopita imekuwa ikipata viongozi wenye sifa ya kuwa viongozi ndio maana jamii ikawakubali na kuwapa ridhaa ya kuwa viongozi. Katika kuiongoza jamii ya watu wapatao takribani watu milioni 44.9 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2012 changamoto ni lazima.
Zimejitokeza changamoto nyingi kubwa na ndogo katika awamu nne zilizopita. Kila awamu na changamoto zake, kila awamu na jitihada zake katika kuikwamua nchi dhidi ya changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hali kisiasa iwe shwari kuilingania nchi swala la amani, upatikanaji wa huduma za afya na mahitaji muhimu pia swala la nchi kuingia  uchumi wa kati.
Tanzania imekuwa mpya, mfumo wa maisha umebadilika, serikali ya awamu ya tano badilisha mfumo wa maisha kuanzia ngazi ya familia serikali za mitaa mpaka serikali kuu imekuwa tofauti na awamu nne zilizopita.
MAJALIWAPMWaziri Mkuu mhe. Kassim Majaliwa.
Ulipaji wa kodi.
Serikali ya awamu ya Tano ni serikali tofauti kidogo na awamu zingine zilizopita, si kwamba awamu zingine wananchi hawakulipa kodi na mashirika binafsi hayakulipa kodi hapana. Serikali ya awamu ya Tano ni serikali inayofuatilia kwa kiasi kikubwa swala la kodi. Shirika la fedha la kimataifa (IMF) limelipoti kuwa.Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara. Haya ni matunda ya ukusanyaji wa kodi na utumiaji sahihi wa mapato yanayokusanya na mamlaka ya mapato TRA. Hivyo tumehama katika kutegemea wahisani na nchi imekuwa ikiendeshwa kwa kodi za wananchi.
 Uwajibikaji.
Tanzania imekuwa nchi ya uwajibikaji kwa kila mwananchi, kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla kila mmoja anawajibika katika nafasi yake. Pesa imekuwa ngumu kwa asiyewajibika kufanya kazi, kwa wale walijikita katika shughuli mbali mbali za halali wanaona hali ya kawaida tu bali ugumu ni kwawale walijipatia pesa kwa njia za ujanja ujanja mambo yamekuwa magumu. Awamu ya Tano imebaini mradi wa wafanya kazi hewa serikalini, ubadhirifu wa fedha za umma katika setka mbali mbali na mashirika yenye umri mrefu katika utendaji bila kulipa kodi.
uchapakazi.
Tanzania ya awamo ya Tano ni Tanzania ya uchapakazi, mwanachi asiye na sifa ya uchapakazi basi katika awamu hii lazima ataona ugumu wa maisha. Watumishi wa serikali wasio na sifa hii ndio wanawakati mgumu. Mashirika binafsi pia kwani kigezo cha kodi kinamuwajibisha kila mmoja kuivaa sifa ya uchapakazi. Rekodi ya muheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuanzia kipindi ni waziri ni uchapakasi na kasi aliyoanza nayo ni uchapakazi. Uchapakazi wa muheshimiwa Rais una hamasisha viongozi na wananchi kwa ujumla kuwa wachapakazi, hivyo tuipata Tanzania mpya ya uchapakazi katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
Maadili.
Tanzania ya wamu ya Tano ni Tanzania inayomulika ipasavyo swala la maadili kwa jamii. Katika mitandao ya kijamii kipindi cha nyuma wanajamii walikuwa wakitumia vyombo hivyo bila kuhofia mkono wa serikali. Awamu ya Tano imeshawatia nguvu wavunja amani mtandano kwa kutoa maneno ya uchochezi, taarifa za uzushi na matusi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga mei 20 mwaka huu kwa kosa la kuto kuwa na maadili mema kwani Kitwanga alishiriki shighuli za kibunge akiwa amelewa. Hivyo tunaipa sura ya Tanzania mpya sasa.
kujitegemea.
Serikali ya Awamu ya Tano iliwashtua wananchi baada ya mheshimiwa Rais kukataa baadhi ya misaada kutoka nje. Tanzania mpya inamjengea mtanzania hali ya kujitegemea kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa kwaujumla. Nchi inayotegemea misaada ya kutoka nchi zilizoendelea, itaendelea kunyonywa kiuchumi na kila siku itakuwa nyuma kiuchumi. Hakuna Taifa lililokuwa kiuchumi kwa kutegemea misaada. Mapato ya nchi ndio yanakuza uchumi wa nchi.
Na Salum Milongo,
0652262797

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top