Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kagera umelalamikia
kitendo kinachofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kutumia janga la tetemeko la ardhi mjini hapa kufanya siasa na
propaganda potofu.
Pia
umoja huo umeitaka na kuishauri Serikali kuacha kazi ya uhakiki,
ugawaji wa misaada yote kwa waathirika ifanywe na askari wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alimueleza suala hilo Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu, alipomtembelea ofisini kwake.
Alimweleza
kuwa kinachofanywa na Chadema ni kituko na fedheha ya kisiasa. Alisema
baadhi ya viongozi wa chama hicho wanatumia tetemeko hilo kujaribu
kujijenga kisiasa huku wakiwabagua wanachama wa CCM kwa itikadi za
kisiasa.
Alisema
uhakiki na utoaji wa msaada katika awamu ya kwanza ulifanyika kukiwa na
ubaguzi na upendeleo huku baadhi ya shehena za mizigo ya misaada na
vifaa vya ujenzi ikiandikwa maneno “ukawa pamoja”.
Wakati
huo huo umoja huo umekikabidhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )