Wakati Rais wa Uturuki, Recep Erdogan
akitua nchini leo, uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania umesaidia
kukua kwa biashara kutoka Dola66 milioni za Marekani (zaidi ya Sh 135
bilioni) hadi Dola180 milioni (zaidi ya Sh360 bilioni).
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa
Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mustafa Efe Uzman ilisema kushamiri
huko kuliongezeka zaidi katika kipindi cha mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam juzi, Uzman alieleza kuwa Uturuki inaamini uhusiano
huo utainua hadhi ya Watanzania ambao nchi yao ni miongoni mwa mataifa
yanayokua kiuchumi katika Afrika Mashariki.
“Sehemu ya uhusiano wa kiuchumi kwa
pande hizi inajumuisha safari za ndege za moja kwa moja za kutoka
Istanbul hadi Dar es Salaam,” alisema katibu huyo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )