Baadhi
ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama
wao Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa
kama sababu za kujivua kwake.
Kwenye
kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini
Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na
haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo
ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa
safari.
“Lawrence
Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu
na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na
wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni
uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema.
Naye
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema
wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja,
na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.
“Tunaojua
sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni
danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa
CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani
na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena
si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.
Pia
Katibu Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA
ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za
yeye kuondoka.
“Mheshimiwa Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa kilichotokea”, ameandika Mashinji.
Lawrence
Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama
hiko hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya
upinzani huwa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )