Mwanamitindo
Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi
aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi
huo umetolewa jana Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa
Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond
aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto
akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si
sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto
anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi
na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter
Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )