Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameeleza wanatilia shaka kuwa mtuhumiwa alitumwa na Lugumi kukwamisha mchakato wa mnada, kwani mazingira ya mnada, na namna mtuhumiwa aliyokuwa anataja bei yanawafanya kuamini kuwa aliwekwa ili wanunuzi wengine wasiweze kununua nyumba hizo.
“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyike ingawa sina fact za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana-top bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” amesema Mambosasa.
“Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji
na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo
akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia
kwa mahojiano,” aliongeza na kusema jeshi hilo linaendelea kumshikilia
Louis kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa
mahakamani.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )