Wafuasi
12 wa Chadema waliokamatwa juzi usiku Kwa kosa la kumshambulia mgombea
wa udiwani wa kata ya Muriet, Francis Mbise wanatarajia kufikishwa
mahakamani kesho.
Wafuasi
hao akiwemo Kaimu Katibu wa Chadema wilayani Arusha, Innocent
Kisanyage walishikiliwa juzi na polisi eneo la FFU Kwa Morombo
wakidaiwa kumshambulia mgombea huyo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mbali na polisi kuwashikilia wafuasi hao pia gari la matangazo linalotumika katika mikutano mbalimbali ya kampeni lilishikiliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Leo Novemba 5 Kamanda Polisi mkoani Arusha
(RPC), Charles Mkumbo amesema kwamba wafuasi hao wote 12 watafikishwa
mahakamani kesho.
Hata
hivyo, Kamanda Mkumbo alipoulizwa kuhusu gari la matangazo
lililoshikiliwa siku ya tukio hakuweza kukiri au kukataa endapo
wameliachia gari hilo na kufafanua kwamba wao hawana shida na gari hilo.
"Sisi tumekamata watu na hatuna shida na gari la matangazo kwani tumekamata watu au gari" amesema Mkumbo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Filed Under:
KITAIFA