Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.
Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana.
"Ni
kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana na kupelekwa kituo cha polisi
cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri
polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka
Oysterbay," amesema Anastazia.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa
amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri
atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )