Mbunge
wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshangazwa na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa kushindwa kuona uhalisia au uongo kwenye ushahidi
waliouwasilisha dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander
Mnyeti na badala yake,wameona siasa.
Nassari
amesema hayo ikiwa ni siku moja kupita baada ya TAKUKURU kutupilia
mbali ushahidi wao kwa kudai kwamba uliharibiwa kwa kuingiza siasa.
Nassari
amesema kwamba “Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka. Cha
ajabu hawajaona uhalisia au uongo uliopo kwenye ushahidi, badala yake
wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata
ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na
aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo
mzima wa Siasa za nchi," Nassari.
Nassari
amefafanua kwamba katika kuwasilisha ushahidi wa kununuliwa kwa
madiwani aliwakabidhi moja ya kifaa alichotumia kurekodia baadhi ya
matukio.
"Niliwapa
takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya
ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya
juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo
zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo".
Ameongeza Nassari
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )