Diamond Platnumz na meneja wake, Babu
Tale jana walikuwa wakihojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM
na kupitia Heka Heka alishare mambo mengi ambayo watu hawayafamu.
Muimbaji huyo alidai kuwa kabla
hajatoka kwenye muziki, alikuwa anapenda sana kuimba wimbo wa Z-Anto,
‘Binti Kiziwi’ kiasi cha watu wengine kuamini yeye ndio Z- Anto.
"Kariakoo nzima ilikuwa ikijua kuwa mimi ndiye Z_Anto nimekula sana chipsi na lift lift "
Alisema ikatokea msichana mmoja
akampenda akijua anayempenda ni Z-Anto lakini baada ya video ya wimbo
huo kutoka, watu wakamjua kwamba sio yeye.
Anadai kuwa baada ya kujulikana
ukweli huo, ilibidi asiendelee kukatiza maeneo ya Kariakoo aliyokuwa
akiyatumia kukaa mara nyingi na kumchukua wiki tatu bila kwenda huko.
Alisema siku alipokutana na binti huyo aliyempenda kwa kudhania ni Z-Anto, alibadilisha njia fasta kwa kuhofia kuumbuka!
"Ilinibidi nikikutane naye nabadilisha njia ama najikausha kuonesha kuwa wajinga ndio waliwao"
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )