Agnes akimfanyia upasuaji dada yake ili atoe watoto baada ya mkunga na wauguzi kukataa kutoa huduma.
Douala, Cameroon
Na Joe Dinga Pefok
WATU
watano wamekamatwa wakituhumiwa kusababisha kifo cha mama mmoja
aliyejulikana kwa jina la Monique Koumate na watoto wake mapacha
Jumamosi, iliyopita huko Douala nchini Cameroon.
Waliokamatwa ni mkunga wa hospitali
hiyo, wauguzi wawili, mhudumu mkuu wa chumba cha kuhifadhia maiti
‘Mortuary’ na mdogo wa marehemu Koumate.
Mwili wa Koumate ukipelekwa mochwari.
Taarifa za awali zilizotolewa na
mashuhuda wa tukio hilo zinaeleza kuwa, mwanzoni Koumate alifikishwa
hospitali akiwa katika hali mbaya akisaidiwa na mdogo wake aliyejulikana
kwa jina la Agnes.
Wakati mama huyo anafikishwa hospitalini
hapo hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa kwenye hatua za mwisho za
kutaka kujifungua, wahudumu wa afya waliokuwa zamu walikataa kumsaidia
kwa sababu hakuwa na pesa kwa ajili ya kulipia huduma.
Agnes alijitahidi kuwasihi wahudumu hao
wamsaidie dada yake kwani atawalipa baadaye kwa kuwa hakwenda na pesa
lakini waliendeleza msimamo wao kwamba mpaka alipie kwanza ndipo
watamsaidia kumzalisha.
Wananchi wakiwa eneo la hospitali hiyo kushuhudia tukio hilo.
Kutokana na kukosa msaada, Koumate
alifariki muda mfupi baadaye na baada ya kuona dada yake ameaga dunia,
Agnes aliwaomba tena wahudumu hao wamfanyie upasuaji marehemu ili
kuwaokoa watoto waliokuwa tumboni ilihali wakisikika kucheza, hivyo
ikadhihirisha bado ni wazima lakini wahudumu wale walisisitiza walipwe
kwanza ndipo watoe huduma hiyo.
Agnes alichukua jukumu la kuchana tumbo
la marehemu dada yake ili aokoe wale watoto mapacha ambapo alifanikiwa
kumtoa mtoto wa kwanza akiwa amefariki, wa pili akawa mzima lakini
baadaye naye alifariki..
Usafi ukifanyika kwenye eneo ambalo Agnes alimfanyia dada yake upasuaji.
Taarifa zingine kutoka Hospitali ya
Laquintinie zilieleza kuwa, Koumate alifikishwa hospitalini hapo akiwa
tayari ameshafariki dunia na ndiyo maana mkunga na wahudumu walipuuza
kumpeleka wodi ya wazazi.
Wahudumu walieleza kuwa mwili wa
marehemu ulitakiwa kupelekwa mochwari lakini Agnes alisisitiza kuwa,
mwili wa marehemu dada yake lazima ufanyiwe upasuaji ili kutoa wale
watoto.
Angalia Agnes alivyomfanyia upasuaji dada yake ili anusuru mapacha;
Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa,
Agnes alipuuzia ushauri wa wahudumu na kuamua kupasua tumbo la marehemu
dada yake chini ya veranda na kukuta watoto wote wawili wamefariki.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Koumate
alikuwa akiishi Douala V na mwanzoni alipelekwa na dada yake kwenye
hospitali ya Wialaya ya Nylon huko Douala III na baadaye baada ya hali
yake kubadilika ilibidi Agnes amhamishie Hospitali ya Laquintinie ambapo
mauti yalimfika
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )