Beki wa pembeni wa Azam FC, Shomari Kapombe.
Na Ibrahim Mussa
Amefunguka kuwa licha ya kufanikiwa kufunga bao lake la nane katika mchezo wa juzi Jumatano dhidi ya Stand United, bado analikumbuka bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Yanga ambalo lilikataliwa.
Amefunguka kuwa licha ya kufanikiwa kufunga bao lake la nane katika mchezo wa juzi Jumatano dhidi ya Stand United, bado analikumbuka bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Yanga ambalo lilikataliwa.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye
Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Kapombe alifanikiwa kufunga
bao pekee na kufikisha mabao nane sawa na John Bocco, mshambuliaji wa
Azam FC ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kapombe
alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya aendelee kufunga mabao mengi ni
kutokana na kitendo chake cha kucheza kwa kujituma ili kuhakikisha
wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara licha ya kuachwa na Simba
kwa tofauti ya pointi nne.
“Nadhani suala kubwa lililopo ambalo
limekuwa likinisaidia katika kufanya vizuri ni kumuomba Mungu na
kujituma hakuna kitu kingine zaidi ya hicho kwa sababu ushindani umekuwa
mkubwa kila timu inahitaji ipate matokeo sasa lazima tupambane ili
kufikia malengo.
“Unajua kwa sasa kufunga kwangu nadhani
ni kitu muhimu katika kila mchezo ili niweze kufanikisha hilo japokuwa
bao nililofunga katika mchezo dhidi ya Yanga lilikataliwa sijui kwa
nini, maana huenda sasa yangefikia tisa,” alisema Kapombe.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )