Aliyewahi
kuwa Mbunge wa Same Mashariki ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mteule wa
Shinyanga, Anna Kilango Malechela, amesema jitihada zake na utendaji
katika kuihudumia jamii ndio sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli kumpa
nafasi ya kuuongoza mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza
kupitia Kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Malechela amedai hata
‘anguko’ lake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, aliangushwa na watu
wenye sababu binafsi na si kukataliwa na Wananchi.
“Mungu
ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais
akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na
kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada.
“Unajua
wanaosema tunabebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa upana
zaidi, wengine tuliangushwa, naahidi kutumia kauli mbiu ya kazi tu
kuitumikia Shinyanga” Alisema Mama Anna Kilango.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )