Jana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli
alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.
Kipindi
cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi
ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia
kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia
nyadhifa hiyo.
“Unajua
kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu
mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono
katika nafasi hii.
“Haijanishtua
kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu
wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri
wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.
Mpaka
kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi
ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na
Mbeya.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )