Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda
maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea
mwenendo wa jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja
kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na
majambazi.
"Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.
"Kuna watu wengi wana silaha halali na wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.
"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.
"Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )