UNA mshkaji anaitwa Mwami Radjabu, wadau wanamtaja kama
kijana mwenye uraia wa nchi jirani ya Kongo (DRC), kwamba
ni mfanyabiashara mwenye ukwasi wa kutosha. Kutokana na mkwanja
wa kutosha alionao, ana ukaribu na akina dada wengi wa Kibongo, hasa
hawa wenye majina katika tasnia ya filamu, wenyewe tukiwajua zaidi
kama Bongo Muvi.
Leo utasikia akitajwa kama Mkongo
wa Wolper au wa Masogange, kesho yake watasema ameporwa na
Hamisa Mabeto, mara utasikia sasa anajirusha na Husna Maulid na
ghafla watasema hivi sasa anatesa na Wema Sepetu.
Na hawa madada wote wanaotajwa, ni
mastaa wetu wanaofanya vizuri katika filamu na uanamitindo. Wamecheza
sinema nyingi na kwa hakika, wanao mashabiki wa kutosha kote nchini.
Kuna msemo unaosema, katika msafara wa mamba na kenge wamo. Usitegemee
kuwakuta mastaa wa fani fulani katika kijiwe cha peke yao.
Kilakiwanja, wanakuwepo wote, Bongo
Fleva, filamu, dansi, mitindo, soka na aina nyingine zote za michezo na
burudani. Kwa maana hiyo, wakati msichana mmoja anapokuwa katika ukumbi
f’lani wa burudani na mtu wake, mastaa wenzake nao wanakuwepo maeneo
hayo, wakifanya yao.
Hivyo
inakuwa rahisi kwa mfano, mwanaume asiyejulikana anayetembea na staa,
kuwafahamu mastaa wengine, kama ambavyo mastaa nao wanavyoweza kumjua
‘shemeji’ yao asiye maarufu. Hiyo inamaanisha kesho akiibuka katika
‘kiwanja’ kingine cha starehe, hata kama hakuwa na mtu wake wa jana,
ataweza kukutana na shemeji zake na kuendelea na makamuzi kama kawa.
Ni hapo ndipo tabu inapotokea. Labda ni
kinywaji, labda ni ofa za maisha mazuri, labda ni mapenzi, lakini
kinachotokea kinakera kukisikia, kwamba mwishowa mchezo, akina dada hawa
wanageukana na kujikuta wote wakiunga ‘cheni’ kwa mtu mmoja. Lakini
kinachosikitisha zaidi ni kusutana kunakotokea baada ya mambo yao
kufahamika.
Ooh huyu ananichukulia
bwana’angu, ananifuatafuata au anikome na kadhalika. Hili siyo jambo
linalopendeza kulisikia kutoka kwa watu ambao jamii inawachukulia kama
kioo.
Katika zamam hizi, hivi kweli watu bado
wanachukuliana mabwana? Licha ya magonjwa, lakini pia haifurahishi kuona
watu tunaoamini kuwa mastaa wakipanga foleni kwa mtu, eti tu kwa sababu
ana pesa.
Hii inaonesha huenda hawana njia
nyingine ya kujipatia kipato zaidi ya kutegemea waleti za wanaume. Kama
hivi ndivyo, niwashauri dada zangu kuachana na staili hiyo ya maisha,
kwa sababu licha ya kujidhalilisha wao wenyewe, lakini pia inaleta picha
mbaya kwa mashabiki na wadau wengine wanaoweza kuwazuia watoto wao
kujiingiza katika fani za umaarufu, wakihofia na wao wataishi
kwa kutegemea wanaume! Dada zangu kuweni makini na Mwami aliyeamua
kuwadilisha kama nguo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )