Kila mtoto anapozaliwa huanza kumuangalia mzazi wake kama ni role model wake, lakini baadaye wengi huanza kubadili mawazo yao.
Mastaa
wa Bongo wameanza kuwatengenezea mazingira watoto wao ya kutembelea
nyota za wazazi wao ili watengeneze hela kuanzia sasa mpaka hapo
baadaye.
Hawa
ni baadhi ya watoto wa mastaa wanaotabiriwa kuja kuwa mastaa baadaye,
wengine wanaweza wakawa na majina makubwa kuliko ya wazazi wao.
Latifa Nasibu (Tiffah)
Mpaka
sasa ana umri wa miezi saba na siku kadhaa, Tiffah amekuwa ni staa pia
ana followers kibao kwenye akaunti yake ya Instagram. Kutokana na
umaarufu aliokuwa nao baba yake, Diamond na mama yake Zari, Tiffah
ameshapata dili kadhaa ambazo zinamuingizia pesa kwa sasa huku akiwa
bado hajui nini kinachoendelea.
Tiffah
ni balozi wa Msasani Mall & Pugu Mall, pia ni balozi wa NMB Junior
Account hii ni akili pekee iliyotumiwa na Diamond Platnumz na Zari
ambayo inaweza ikamfanya Tiffah akatumia fursa hiyo kuja kuingiza hela
nyingi hapo baadaye na akawa maarufu zaidi duniani.
Kendrick Mabeste
Mabeste
na Lisa wanajivunia kuwa na mtoto kama Kendrick, akiwa anakaribia umri
wa miaka mitatu, Kendrick ameshaanza kuwa maarufu na kuingiza mkwanja
wake binafsi kwa kufanya baadhi ya matangazo.
Pia
Kendrick amewahi kuwa mshindi kwenye shindano la Tabasamu akiwa ni
mtoto mwenye kupendeza kwenye picha (Photogenic). Nje ya kufanya
matangazo watu wameanza kumtabiria Kendrick kuja kuwa rapper kama baba
yake (Mabeste).
Tanzanite Hamisi
Madini
ya Tanzanite yana patikana Tanzania pekee, japo nchi ya India ndiyo
inaonekana ni ya kwanza kwenye kuuza madini hayo. H Baba na Flora Mvungi
hawakukosea kumuita mtoto wa jina la Tanzanite, ni mmoja kati ya watoto
wa mastaa wenye mvuto na wenye muonekano mzuri.
Tanzanite
yupo chini ya menejimenti ya Lisa Karl Fickenscher, ambaye anamsimamia
Kendrick pia. Koffie Olomide aliwahi kumweka Tanzanite kwenye Instagram
yake baada ya kushinda shindano ambalo Koffie alilitoa mtu ajirekodi
akiimba wimbo wa Ekotite na kuahidi atakaye shinda angewekwa kwenye
Instagram yake.
Pia
alipata mualiko wa kushiriki mashindano ya U miss kwa watoto ambayo
yalifanyika nchini Rwanda. H. Baba aliwahi kusema “kuwa kuna matangazo
mengi ambayo Tanzanite anatakiwa kuyafanya kwa sasa.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )