Staa wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel Grayson.
Hatimaye staa wa Bongo Muvi, Aunt
Ezekiel Grayson amefanya kila liwezekanalo na kujinasua mikononi mwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli ‘JPM’
kwa kukomboa gari lake aina ya Audi lililokuwa limeshikiliwa na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushindwa kulipa kodi.
Gari la Aunt Ezekiel aina ya Audi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa
mbwembwe kibao wikiendi iliyopita, Aunt alimshukuru Mungu kwa kumnasua
kwenye soo hilo kwani alikuwa akiishi kwenye lindi la mawazo kwa zaidi
ya wiki tatu tangu gari hilo likamatwe.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutoa
shilingi milioni 15 na hatimaye nimekomboa gari langu ambalo lilikuwa
kwenye hatihati ya kupigwa mnada na TRA,” alisema Aunt.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )