Dar es Salaam: Tenda miujiza Bwana! Lile sakata la mwanadada Rehema Charamila ‘Ray C’ kuandamwa na pepo mbaya wa utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ hata baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘JK’ kumsaidia, inasemekana Mwanamuziki Judith Wambura ‘Jide’ ameambatana naye kanisani kwa ajili ya maombi.
Kikimwaga ‘ubuyu’ mbele ya Ijumaa
Wikienda, chanzo chetu kilitonya kuwa hivi karibuni Ray C alitinga
nyumbani kwa Jide, Masaki jijini Dar kwa ajili ya kumsalimia na kumpa
hongera kwa wimbo wake mpya wa Ndi Ndi Ndi, lakini wakati huohuo kukawa
na dada anayefahamika kwa jina la Anitha ambaye huwa anasali na Ray C.
….Wakiwa kwenye pozi.
Ilifahamika kwamba Anitha ni rafiki wa
Ray C na pia wa Jide hivyo ulipofika muda wa kwenda kwenye maombi ndipo
Jide akaungana na Anitha kumpeleka Ray C kanisani kwa ajili ya maombi.
“Jide na Ray C wana muda mrefu sana
hawajaonana kwa zaidi ya miaka mitano au sita ila hivi karibuni Ray C
alikuja nyumbani kwa Jide (Masaki) kwa ajili ya kumsalimia na kumpa
pongezi kwa wimbo wake mpya ndipo Jide alipojumuika kumpeleka Ray C
kanisani kwenye maombi ingawa nasikia kuna watu wengi ambao wanamsaidia
Ray C na muda mwingi anaenda kanisani kwa ajili ya maombi,” kilisema
chanzo hicho.
Kwa upande wake, meneja wa Jide,
Christina Mosha ‘Seven’ alithibitisha Jide kutembelewa na Ray C kisha
kwenda kanisani kwa maombi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )