Sabrina Gharib.
PWANI: Sabrina Gharib, binti mwenye
miaka 19 anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo kwenye Mochwari ya
Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu
wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, Uwazi
limeibuka naye.
“Tulipokwenda kuchukua mwili wa mpendwa
wetu Tumbi, tulisikia watu wakimzungumzia msichana mdogo anayehudumia
maiti. Kwanza sikuamini lakini nilimuona na kwa kweli alituhudumia
vizuri,” alisema Frida John, mmoja wa waliokwenda kuchukua maiti
hospitalini hapo.
Katikati ya wiki iliyopita, gazeti hili
lilikwenda hospitalini hapo likiwa na kundi zima la Global Tv On Line na
kufanya mahojiano naye ambapo Sabrina alisema aliamua kusomea kazi ya
kuhudumia maiti badala ya unesi kutokana na kujua kuwa, ajira kwa fani
hiyo zipo nje nje.
MSIKIE MWENYEWE
“Niliamua kusomea kazi hii kwa kujua kuwa ina soko la ajira. Awali nilikuwa msichana pekee darasani. Siku ya kwanza kusoma kwa vitendo katika Hospitali ya Iringa, nililia kwa sababu niliona kama maiti naiumiza lakini mwalimu wangu aliniambia nisiwe na hofu, mtu huyo amekwishafariki dunia, hivyo hasikii maumivu,” alisema Sabrina.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa
Shirika la Elimu Kibaha, Pwani ambao ndiyo wamiliki wa Hospitali ya
Tumbi, Lucy Semindu, akimuelezea msichana huyo alisema ni jasiri ambaye
amefanya kazi nzuri wakati wa elimu yake kwa vitendo.
“Ameonesha mfano mzuri na kuthibitisha kuwa wanawake wanaweza,” alisema Lucy.
“Ameonesha mfano mzuri na kuthibitisha kuwa wanawake wanaweza,” alisema Lucy.
Naye mmoja wa viongozi katika mochwari hiyo ya Tumbi, Francis Kobelo alisema msichana huyo ni mfano wa kuigwa.
“Ukimwambia fanya hivi, hana hofu, anafanya, inaweza kuja maiti imeharibika ukimwambia fanya moja, mbili, tatu na baadaye ukija kuikagua unakuta amefanya vizuri sana,” alisema Kobelo.
“Ukimwambia fanya hivi, hana hofu, anafanya, inaweza kuja maiti imeharibika ukimwambia fanya moja, mbili, tatu na baadaye ukija kuikagua unakuta amefanya vizuri sana,” alisema Kobelo.
Mama mzazi wa Sabrina, Asha Ramadhani
alipohojiwa alisema siku ya kwanza alipopigiwa simu na binti yake huyo
kumwambia anachukua masomo ya kuhudumia maiti mochwari,
alichanganyikiwa.
“Nilimuuliza unataka kuwa chizi? Lakini
sikuwa na la kufanya, nilimuacha aendelee na masomo yake,” alisema mama
huyo huku akibainisha kuwa, Sabrina ni mwanaye wa kwanza.
Kwa maelezo zaidi na kuona ‘live’ tembelea mtandao, www.globaltv.com ujionee na kusikiliza mahojiano hayo kwa kina zaidi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )