Msanii
wa bongo flava Harmonize anayetamba na wimbo "Bado' ameshangazwa na
namna ambavyo Msanii Diamond Platnumz anavyoweza kuhimili maumivu ya
kimapenzi.
Akizungumza
katika kipindi namba 1 cha burudani nchini (enewz) cha EATV amesema
kuwa suala la mapenzi linaendana kabisa na maisha ya mtu mwenyewe na
yeye hana uwezo wa kuhimili maumivu ya kimapenzi.
"Diamond
sijui ana uwezo gani wa kuhimili maumizu ya kimapenzi na kuwa na
mwanamke wakaenda na anaachane naye, lakini mimi kama mimi sina uwezo
huo"
Hata
hivyo msanii huyo amesisitiza kuwa kwa sasa anatumia muda wake mwingi
kuangalia ni mwanamke gani anayemfaa na hatokuja kuharibu maisha yake.
Ameongea kuwa mwanamke anaweza akakufelisha kabisa au akakupa manufaa.
"Ukiwa
na mwanamke mzuri mkawa mnashauriana vizuri inaweza kukufanya ikawa
chachu ya maendeleo yako, lakini ukiwa na mwanamke mzuri akawa
anakushauri vibaya inaweza kuwa chachu ya kufeli kwako kimaisha" .
Amesema Harmonize.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )