Na John Stephen, MNH
Dar
es Salaam, Tanzania.Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili
LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat
ambaye amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa
moyo wake.
Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri.
Dk
Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa
moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo
ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa
binadamu.
“Upasuaji
huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa
watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa
kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza.
“Tatizo
la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka
mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo. Upasuaji umefanywa kwa
ushirikiano wa madaktari wa moyo na madaktari wa matibabu ya moyo
nikiwamo mimi (Dk. Godwin Sharau), Dk Michael Valentine kutoka
Marekani, Dk Kisenge na Dk Sulende Kubhoja, Dk wa usingizi, Dk Anjelan
Muhozya na madaktari wengine ambao wamesaidia katika upasuaji huu,” amesema Dk Godwin Sharau.
Mama
wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley ambaye ni mkazi wa Sakina-Raskazon
mkoani Arusha amewashukuru madaktari wa Taasisi hiyo kwa kufanya
upasuaji huo na mtoto wake kutoka salama katika chumba cha upasuaji.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )