Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Nikafanya
kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina
ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika
bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na
kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza
kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa
kutufyatulia
Endelea....
Macho
yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote
wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo
pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na
sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma
kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa
bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo
lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na
kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe
yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.
Nikafunga
breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola
zetu zikiwa mikononi,tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya
milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa
zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa
kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye
kona, nikataka kunyanyuka
“eddy kaa chini”
Dorecy
alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga
kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza
kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo
ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama
mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata
“nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“kaza mkono”
Dorecy
alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao
wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya
mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“unafanya nini?”
“ngoja nikuonyeshe”
Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘system weapon empty’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“vipi?”
“kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“ni nini?”
“silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”
Dorecy
alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia
upande niliopo, nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee
godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku
nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye
alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi
hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa
basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”
Nilimuambia
dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi
pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo
nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa
wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria dorecy
kujitokeza, dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri
wajitokeze
Nikaishika
bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu
yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha
nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu,
risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya
tatu ikapiga kwenye tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku
likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua
chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.
Nikashuka
kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta dorecy akiwa bado
ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa
mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha
jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye
hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu
Nikageuka
nyuma na kumkuta dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani
haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi
lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango
na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari
linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia
hadi tukatokea barabara inayotokea tanga kuelekea moshi
“eddy, ulisha wahi kuua?” dorecy aliniuliza
“swali gani sasa hilo?”
“hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“nimefanyaje?”
“ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“kawaida”
Nilimjibu
huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni
barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au
hakuna.Tukaingia kwenye motel iitwayo mombo motel iliyopo kwenye
barabara ya mombo
“una pesa?”
Nilimuuliza dorecy
“ndio”
“kachukue chakula basi”
“utakula nini?”
“bufee,nyama chukua na soda za take way”
Dorecy
akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele
zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa
kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona
askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la motel wakiwa na
pikipiki.
Wakaisimamisha
pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani
sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama
gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi
zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa
“habari yako afande?” nilianza kumsalimia
“salama, gari yako ilipata nini?”
“kivipi?”
“imebonyea pembeni huku?”
“ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”
“sawa afande”
“insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“ahaaa, upo ikulu wewe?”
“yaaa”
“wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“inategemea, na kazi”
“ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“shida gani?”
“ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“wabaneni”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )