Hofu
ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu ambaye
ni mtuhumiwa wa kesi ya uchochezi, imetoweka baada ya mahakama hiyo
kukubaliana na utetezi wa wadhamini wake kuwa, Lissu yupo Ujerumani kwa
matibabu.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, alishindwa kuhudhuria mahakamani siku ya juzi na hivyo wadhamini wake kutakiwa kufika mahakamani jana kujieleza, kwanini mtuhumiwa huyo asifutiwe dhamana.
Kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu ni kesi Na. 208 katika gazeti la MAWIO akiwa ni mtuhumiwa namba nne sambamba na Jabir Idrissa, Simon Mkina, na Ismail Merhaboob.
Jabir ni mwandishi mwandamizi wa MAWIO, Mkina ni mhariri wa gazeti hilo na Merhaboob ni meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti inayojulikana kwa jina la Flint.

Jana,
wadhamini wa Lissu Ibrahim Ahmed na Robert Katula walisimama mbele ya
Hakimu Thomas Simba anayesimamia kesi hiyo, na kusema kuwa Lissu
hakutokea mahakamani kwa sababu amesafiri nje ya nchi kwa ajili ya
matibabu.
Hata
hivyo, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali
Mutalemwa Kisheruji uliiomba mahakama kuzuia hati ya kusafiria ya
mshitakiwa Lissu pamoja na kumuwekea sharti la kuiomba mahakama kibali
cha kusafiria endapo atarudia tena kosa hilo kutokana kwamba hakufuata
sheria kwa sababu alitakiwa kutoa taarifa mapema kabla ya siku ya shtaka
kusikilizwa.
Lakini
Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala na
kuiomba mahakama kutenga siku nyingine ambapo alimuahidi hakimu kuwa
kosa hilo halitajirudia tena na siku husika ya kusikilizwa shitaka
mshatikiwa atakuja mahakamani.
Baada
ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili, Hakimu Simba alitoa onyo kali
kwa mshitakiwa na kuwaambia wadhamini wa Lissu kuwa, endapo siku nyingi
mshitakiwa huyo hatakuja mahakamani, wadhamini watalipa dhamana.
Hakimu
Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba, 4, 2016 baada ya mawakili wa
pande zote mbili kuiridhia tarehe hiyo iwe siku ya kusikilizwa shtaka
hilo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )