Mtunzi: Eddazaria g.Msulwa
Ilioishia
Nikamkabidhi
msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha
hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye
kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya
kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho
makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama
pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza
kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi
kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika
maeneo ya shingoni
Endelea
“vua cheni yako”
Askari
anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa
shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi
chini kwenye miguu,
“safari njema”
Dada
aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku
akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia
tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“asante na wewe pia kazi njema”
Nikapita
kwenye kizuizi na kuwafanya sashah na rajiti kushusha pumzi nyingi
kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari,
tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru mungu, siti zetu tatu zipo
sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge
mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya
dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini kenya
“eddy” rajiti aliniita
“naam”
“unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“kweli?”
“ndio, umekuwa bonge la handsome”
“mmmmm”
“kweli vile”
“jamani acheni kelele watu wamelala” sashah alizungumza
“ahaaa shauri yao, bwana”
Masaa
yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo,
baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari
ikaendelea.Tukafika nchini iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri
huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani
masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari
wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba
sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya
uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura
bandia,
Sikuwa
na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni sashah na
rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja
wa ndege na sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye
mkuta ndani ya teksi hii, tukafika kwenye moja ya hotel kubwa iliyo
andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza
shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya
kiarabu
Sashah
akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja,
akatufwata sehemu tulipo simama na rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo
tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho sashah
alikodisha
“eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu”
Sashah alizungumza
“na nyinyi munakwenda wapi?”
“sisi,
tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni
wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji
utakayo yahitaji tumegharamia”
“sasa jam….”
“eddy
hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza
tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za
kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye
sehemu ya chakula”
“sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?”
“kuna
kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo
sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula
unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya
kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili”
“powa”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )