HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.
Habari za uhakika zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.
“Nilimtembelea
siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake
ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi
kuendelea na majukumu yake.
“Nimesikitishwa
mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua
bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia
mtu kifo sijui inafaidika nini.
“Mpaka
anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na
tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.
Septemba
19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini
alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu
amsaidie.
Siku iliyofuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.
Sitta
ameshika nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka
2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )