. Askofu wa Dayosisi ya
Dar es Salaam wa Kanisa la Anglikana, Dk valentino Mokiwa jana
alishindwa kuendesha vikao viwili baada ya kundi la waumini kufika
Usharika wa Ilala kwa lengo la kuzuia.
Askofu
Mokiwa, ambaye anapinga uamuzi wa Askofu Mkuu wa Anglikana, Dk Jacob
Chimeledya kumvua madaraka kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya
fedha, alikuwa aendeshe vikao vya kamati ya fedha na halmashauri kuu,
lakini alilazimika kuviahirisha baada ya kundi hilo kufika eneo hilo.
Wakati
waumini hao wakizuia vikao hivyo kufanyika, mashemasi, mapadri,
wainjilisti na waumini wa dayosisi hiyo wametoa tamko la kumuunga mkono
Dk Mokiwa wakipinga uamuzi wa mkuu wa kanisa hilo kumvua madaraka.
Askofu
Mokiwa anapinga uamuzi wa kumvua madaraka akisema hauwezi kufanywa na
mkuu wa kanisa, bali na halmashauri kuu ya jimbo ambayo anasema
haikushirikishwa zaidi ya kutaarifiwa uamuzi huo.
Tukio
la jana la kumzuia Dk Mokiwa kufanya mkutano lilitokea saa mbili
asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Nicolau wilayani Ilala, ambako kuna
ofisi ya Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )