.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk
Ali Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana
walihitimisha kampeni za vyama vyao za ubunge wa Dimani ambao uchaguzi
wake unafanyika leo kila mmoja akitamba kushinda.
Dk Shein ambaye ni Rais wa Zanzibar,
akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Fuoni alirejea kauli
yake kwamba hakuna umoja wa mataifa au nchi yoyote inayoweza kumuondosha
madarakani.
Dk Shein alisema hayo akiendelea kujibu
kauli ya Maalim Seif kwamba siku si nyingi kutatokea mabadiliko makubwa
na kwamba wanachama wake wasifadhaike.
Dk Shein alisema CUF walikataa wenyewe
kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016,
hivyo wanabaki wakitangatanga, “...Wasahau kabisa kuipata nafasi ya
urais wa Zanzibar. Hawana uwezo hata wa kuongoza udiwani sembuse urais.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )